CWT Ilala yaililia serikali kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara.
Na Mussa Augustine.
Chama cha Walimu Nchini (CWT) Jiji la Ilala kimeiomba serikali kulipa madeni ya walimu ikiwemo malimbikizo ya mishahara pamoja na fedha za likizo kwa walimu wastaafu sanjari na waliopo kazini.
Ombi hilo limetolewa na Katibu wa chama hicho Wailaya ya Ilala Bwa. Erasmo Mwingira wakati akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ambayo yamelenga kuwawezesha kutambua haki zao,uwajibikaji pamoja na maadili ya kazi yao.
Mwingila amsema kwamba pamoja na chama hicho kupata manufaa makubwa lakini kuna baadhi ya changamoto ambazo zinawakumba walimu ikiwemo kusua sua kwa ulipaji wa malimbikizo ya mishahara huku wakiahidi kwamba wanaendelea kushirikiana vyema na serikali.
" Ndugu mgeni rasmi tunaishukuru serikali kuwapandisha madaraja baadhi ya walimu,lakini tunaomba pia walimu wanaodai madeni ya likizo na uhamisho,jumla ya kiasi cha shilingi 2504058165 na kati ya fedha hizo madeni ya walimu wa msingi ni 1522218881 na sekondari ni shilingi 981839284,serikali ilipe fedha hizi ili kuondoa changamoto zinazowakumba walimu" amesem Bw.Mwingira.
Kwa Upande wake Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Frank Sanga amesema kwamba maombi hayo atayafikisha sehemu inayohusika nakwamba changamoto hizo zitafanyiwa kazi.
" Ndugu zangu nimewasikiliza kupitia risala yenu,mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Ilala yupo kwenye ziara hivyo kanituma nije kumuwakilisha,haya maombi yenu nimeyachukua,nitayafikisha sehemu husika,nimefurahishwa sana na mafunzo haya mnayoyapata leo natumaini yatawasaidia sana katika utendaji wenu wa kazi" amesema Bw.Sanga.
Nae Kaimu afisa elimu Sekondari Bi.Aziza Sasi amewataka wawakilishi hao wa wawalimu kuhakikisha wanazingatia mafunzo hayo ambayo yameanza leo Okotoba 5 hadi okoba 6 ,2021 ,nakwamba yatawasaidia katika utendaji wao,kujua haki zao na wajibu pamoja na kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni