Zinazobamba

MCHONGOO KUBADILISHA MFUMO WA AJIRA

 Na Fatma Ally, Dar es Salaam

Jukwaa la  mtandao wa utoaji wa huduma,  Nchini Tazania limesema limejipanga kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana ambapo limelenga  kuunganisha vijana wenye ujuzi vipaji na elimu mbalimbali  na  watoa huduma, na wanaotafuta huduma kama njia ya kuweza kujikwamua kimaisha.
Baadhi ya viongozi wa wa Tasuba wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Jukwa la mtandano wa katikati Julius Wabongo, wakwanza kulia ni Cheif Instructor Gabriel B Liza na wa mwisho kushoto ni Principal Dr Herbert F Makoye.
Katika taarifa iliyotolewa na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Jukwaa hilo, Julius Wambogo,  amesema wanatumia teknolojia ya digitali ikiwa ni njia mpya ya kupata na kutoa huduma zinazosaidia kufanya kazi katika maisha ya kila siku na kwa haraka zaidi na kutoa matokeo chanya.

Amesema kuwa, pamoja nakuwa wazi kwa sasa wanapanga kuzindua rasmi mapema mwakani 2022, na itawagusa watu binafsi, makampuni, miradi ya shirika na ya viwandani, kwenye mtandao wa watoa huduma wenye ujuzi, wabunifu ambao wana utaalamu katika sekta mbalimbali katika nyanja za kazi ili kuungana na kufanya kazi kwa urahisi.

Aidha, amesema  katika kufanikisha hilo watu hao wataunganishwa na watoa huduma na wanaotafuta huduma na kujumuisha biashara zote, mashirika, na vyama katika ngazi za kitaifa, kikanda, na bara.

Hata hivyo, ameeleza kuwa Mchongoo ni jukwaa linalowaunganisha watoa huduma mbalimbali hatua itakayotoa fursa mbalimbali.

Mchongoo.com inakusudia kukusanya watoa huduma kuboresha utafutaji huo ili kutoa mahali ambapo kuna wenyeubunifu, wenye talanta na wenye uzoefu ambao wanaweza kuonyesha ujuzi wao na ili waweze kupatikana kwa urahisi.

Ameongeza  kuwa, Mchongoo ni huduma aina zote hutolewa kupitia jukwaa hilo la mtandaoni kwa kushirikiana na sekta binafsi, wizara na mataifa yenye dhumuni la kukuza uchumi wao na kuimarisha ubunifu pamoja na kuondoa umasikini katika jamii na kwamba mtandao huo ni muongozo.

"Kila mwaka kampuni ufanya  mambo tofauti ili kuongeza mauzo na shughuli zao, kusaka wajuzi na wataalam ila wanatumia nguvu nyingi na mitandao mingi sababu hakuna sehemu moja wanayopatikana na mara kwa mara wanatakiwa"amesema 

Amebainisha  zaidi kuwa dhumuni jingine ni kubadilisha soko la kazi na utoaji wa huduma na kujenga tena kile kilichoathiriwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na Uviko-19.

“Mchongoo tunahitaji msaada wako na ushirika wako wasiliana nasi ili kujitolea au kuwekeza asannte, hivyo kupitia teknolojia tumekusudia kubadilisha soko la ajira na utoaji huduma kwa kuboresha namana ya uapatikanaji, hii ni kutokana na athari mbalimbali zilizochangia kuyumba kwauchumi ikiwemo ugonjwa wa Corona,”amesema Wambogo.

Ameongeza kuwa, kila mwaka zaidi ya wahitimu 1,000 humaliza masomo yao huku wengine zaidi ya 1,000 pia wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa fedha.

Amesema kuwa, pamoja na kwamba wanafunzi hao wanashindwa kuendelea na masomo makampuni mengi huingia sokoni kutafuta wataalamu mbalimbali kila mwaka baadhi ya makampuni bila mafanikio yakupata wanacho tafuta na kusahili.

“Utafutaji huu huchukua muda na nguvu ya watendaji wa makampuni kwani uhitaji wa wataalamu unakuwa mkubwa,”amesema Wambogo.

Aidha amesema kuwa jukwaa la https://mchongoo.com itakuwa ni sehemu ya kutatua changamoto mbalimali za ajira kwa vijana na utafutaji ya watoa huduma wabunifu, wenye ujuzi na elimu wataonyesha ujuzi wao na kupatikana kwa urahisi kwaunganisha na watafuta huduma binafisi na makampuni yenye uhitaji.

Hakuna maoni