IFAHAMU SIMU TISHIO KUTOKA INFINIX
Hivi
karibuni kampuni ya Infinix imeingiza sokoni simu mpya ya Infinix Zero X Pro
simu ambayo tumeisikia sana kwenye habari mbalimbali, kwa upande mwingine
kampuni ya Vivo nayo pia siku za nyuma ilizindua simu yake mpya ya Vivo Y53s.
Kupitia
makala hii tutaenda kuangalia tofauti kubwa za simu hizi mbili kwa upande wa
sifa, muonekano na mengine ya muhimu. Na tumaini kuwa hadi mwisho wa makala hii
utaweza kujua ni simu gani ambayo ni bora kwako.
Muonekano
Ni
kweli kuwa Infinix Zero X Pro na Vivo Y53s zote zina kuja na muonekano mzuri
lakini ni wazi kuwa Infinix Zero X Pro inakuja na muonekano bora na wa tofauti
sana.
Hii
ni kutokana na muonekano wake wa nyuma ambao haupatikana kwenye simu nyingi za
sasa.
Ni
wazi kuwa kwa upande wa muonekano Infinix Zero X Pro ina muonekano wa tofauti
kuliko Vivo Y53s. Hii ni kutokana na muonekano wa Vivo Y53s kutumika kwenye
simu nyingi sana.
Kioo
Infinix
Zero X Pro inakuja na kioo cha inch 6.67, wakati Vivo Y53s inajua na kioo cha
inch 6.58. Wakati infinix Zero X Pro ikiwa na kioo kikubwa kwa upande wa size
ya kioo, lakini pia Infinix Zero X Pro inakuja na kioo bora cha AMOLED chenye
kuonyesha rangi vizuri zaidi tofauti na kioo cha IPS LCD ambacho kina tumika
kwenye simu ya Vivo Y53s.
Kwa
upande wa kioo ni wazi kuwa Infinix Zero X Pro ni bora zaidi kwani kioo cha
AMOLED ni bora sana kuliko kioo cha IPS LCD hasa kwenye upande wa rangi.
Mbali
na hayo kioo cha infinix Zero X Pro kina resolution ya 1080 x 2400, wakati Vivo
Y53s ina 1080 x 2408.
Tofauti
nyingine kubwa ambayo inapatikana kwenye simu ya Infinix Zero X Pro ni pamoja
na kuwa kioo cha simu hii kina kuja na 120Hz Refresh rate wakati Vivo Y53s
haina teknolojia hii kwenye kioo chake.
Kamera
Kwa
upande wa kamera hapa ni wazi kuwa Infinix Zero X Pro imeshinda kwa kuwa simu
hii inakuja na teknolojia ambayo haipo kabisa kwenye simu ya Vivo Y53s.
Mbali
ya kuwa kamera za Infinix Zero X Pro ni kubwa zaidi lakini pia kamera hizi zina
uwezo mkubwa zaidi.
Kama
unataka kupiga picha za tofauti ambazo pia utaweza kuzoom vitu kwa ukaribu
zaidi basi kamera hizi tatu (Megapixel 108, MP 8, MP 8) za Infinix Zero X Pro
ni bora zaidi kwako. Hii ni kutokana na kamera hizi kuwa na uwezo wa 60x
Periscope Lens ambayo inaweza kuzoom vitu kwa ukaribu zaidi, ikiwa pamoja na
uwezo wa kupiga picha Mwezi na kufanya uonekane karibu zaidi.
Kwa
upande wa Vivo Y53s unapata kamera tatu pia ambazo zinakuja na Megapixel 64 na
nyingine mbili ambazo zina Megapixel 2 kila moja.
Mbali
na hayo kamera za Infinix Zero X Pro kwa pamoja zinaweza kuchukua video za 4K,
wakati kamera za Vivo Y53s zinaweza kuchukua video za hadi 1080p pekee.
Pia
tofauti nyingine ni kuwa Zero X Pro inakuja na flash ya Dual-LED flash kwa
mbele, wakati Vivo Y53s haina flash kwa mbele.
Sifa za Ndani
Kwa
upande wa sifa ni wazi kuwa Infinix Zero X Pro inashika namba moja hii ni
kutoka na kuwa simu hii inatumia processor yenye chipset ya Mediatek Helio G95,
wakati Vivo Y53s inatumia chipset ya Mediatek Helio G80 ambayo ni ndogo.
Mbali
na hayo Infinix Zero X Pro inakuja na CPU yenye speed zaidi ya Octa-core
(2x2.05 GHz Cortex-A76 & 6x2.0 GHz Cortex-A55), wakati Vivo Y53s inakuja na
CPU yenye Octa-core (2x2.0 GHz Cortex-A75 & 6x1.8 GHz Cortex-A55).
Ni
wazi kama wewe ni mpenzi wa game basi simu ya Infinix Zero X Pro itakufaa zaidi
kutokana na kuwa na chipset bora zaidi kwa game, bila kusahau CPU yake pia
inakuja na speed zaidi kuliko Vivo Y53s.
Battery
Kwa
upande wa battery Vivo Y53s inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh, wakati
Infinix Zero X Pro inakuja na battery ya 4500 mAh. Mbali ya hayo simu ya
Infinix Zero X Pro inakuja na teknolojia bora ya Fast charging ya hadi 45W
ambayo kwa mujibu wa Infinix inaweza kujaza simu yako hadi asilimia 40 ndani ya
dakika 15 pekee.
Hitimisho
Ni
wazi kuwa simu ya Infinix Zero X Pro ni simu bora kuliko Vivo Y53s, hii ni
kutokana na kuwa na muonekano bora na watofauti, kioo bora zaidi cha AMOLED,
kamera kubwa ya Megapixel 108 yenye uwezo wa kuchukua picha za bora, pamoja na
processor bora ya Mediatek Helio G95, bila kusahau uwezo mzuri wa kujaa chaji
kwa haraka kutokana na teknolojia ya Fast charging.
Kwa
maoni yangu binafsi, Vivo Y53s na Infinix Zero X Pro ni simu ambazo zote
zinauzwa bei zinazo fanana, hivyo kama unahitaji sifa zaidi na uwezo zaidi basi
Infinix Zero X Pro ni simu bora zaidi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni