Waziri Makamba: TANESCO kuwa Shirika la kutoa huduma na kibiashara
Na Mussa Augustine.
WAZIRI wa Nishati January Makamba amewataka wafanyakazi wa shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuanzia sasa wafanye kazi kwa weledi ili kulifanya shirika hilo liwe na mapinduzi makubwa nakuweza kuwa na thamani barani Afrika.
Waziri Makamba ametoa maelekezo hayo jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano na Mameneja wa TANESCO wa kanda, Mikoa na Wilaya pamoja na Mameneja wa vituo vya kufua Umeme na wafanyakazi wa shirika hilo.
Amesema kwamba shirika la TANESCO kufuatia mabadiliko ya Uongozi yaliyofanywa na rais Samia Suluhu Hassan ya kutengua na kuteua Mkurugenzi Mkuu mpya wa shirika hilo,Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, pamoja na kuivunja bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo ni ishara tosha kua serikali inataka shirika hilo lijiendeshe kibiashara na kihuduma zaidi hivyo wanapaswa kua na mtazamo huo.
"kuanzia sasa shirika hili litaongeza mapato serikalini ,litawajali watumishi na wateja wake ,liwe na thamani ndani na nje ya Nchi za afrika,nakwambia liheshimike kutokana nakwambia nishirika ambalo linaingiza mapato makubwa kwa mwaka ya shilingi trilioni 1.8,na kwamba lina aseti zenye thamani ya trilioni 13 ambayo ni kiwango kikubwa ukilinganisha na mashirika mengine" amesema Waziri Makamba.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimari watu wa Shirika hilo Frances Sangunae mesema watatoa ushirikiano mkubwa kwa bodi ya shirika pamoja na menejimenti zingine ili kufikia malengo ya shirika ambalo malengo makubwa ni kulifanya liwe na ustawi mkubwa nakuweza kujiendesha vizuri katika kutoa huduma kwa wananchi.
Kamishna mpya wa Umeme na Nishati Jadidifu Injinia Felschesm Mramba amesema kwamba sekta ya Umeme inaenda kubadilika na kupata matokeo mazuri,hivyo kutokana nakwambia Mameneja wengi wanajua matatazo ya shirika itakua rahisi kutatua changamoto hizo.
"Maeneo muhimu ya kuanzia ni kama aina ya wateja wetu na idadi yao,pia uzalishaji wa wafanyakazi wetu, ukusanyaji wa mapato,kwahiyo bodi ya tanesco mkiyaona haya yanaweza kutusaidia kufanya vizuri zaidi" amesema Injinia Mramba.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANESCO Bw Maharage Chande amesema atafanyakazi lakini amewasisitiza watoe huduma nzuri kwa wateja lakini pia kushirikiana kutataua changamoto zinazolikumba Shirika ikiwemo kukatika Umeme na kuwathamini wafanyakazi kulingana na utendaji wa kazi kwenye nafasi yake.
"Safari hii ya shirika letu ni ngumu Sana tusijidanganye tujiandae kisaikolojia kwamba katika utendaji wetu wa kazi tutakumbana na changamoto hivyo tuwe tayari kukabiliana nazo,safari yetu haitakuwa ya asali na maziwa yaaani raha tu ,mjue tutakuwa na changamoto mjiandae kukabiliana nazo" amesema.
Omary Issa mwenyekiti mpya wa bodi ya wakurugenzi TANESCO,amesema kwamba bodi nyingi zimekua na mwingiliano wa majukumu,hivyo waziri ametuhakikishia kwamba bodi yetu itakua bodi huru lakini inafanya kazi kutimiza kazi za wadau ambao ni serikali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni