Zinazobamba

WAJASIRIAMALI WA SOKO LA BUNJU "B" WAFIKIWA NA MAFUNZO YA ABCD KUTOKA TGNP.

Na. Vicent Macha, Dar es salaam

Wakina Mama wengi wa kata ya Mabwepande wanamwamko mkubwa wa kufanya biashara lakini wanakwama kwa kukosa elimu sahihi ya ujasiriamali na matokeo yake wanapoteza mitaji yao na kubaki kulaumu na kusingizia chuma ulete.

Diwani wa kata ya Mabwepande Mh. Muhajirina Kasim akielezea umuhimu wa mafunzo hayo mapema jana kwenye soko la Bunju "B" mkoani Dar es salaam.
hayo yameelezwa mapema leo mkoani Dar es salaam na Diwani wa kata ya Mabwepande Mh. Muhajirina Kasim wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali wa soko la Bunju "B" lililopo kwenye kata hiyo.

Diwani huyo amesema kuwa wafanya biashara wengi hasa wamama wanakuwa na mipango mizuri, lakini wanashindwa kuitimiza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa elimu sahihi ya biashara hivyo kusababisha kupoteza mitaji yao.

Ameendelea kusema kuwa miongoni mwa elimu aliyoipata leo ni Mila na Desturi zilizopitwa na wakati zinavyoweza kukwamisha ustawi na ukuaji wa mtoto wa kike, kwani mila hizi zinaweka mipaka kwa mzazi wa kiume kutojihusisha na Mambo yanayomuhusu mtoto wa kike ikiwemo masuala ya hedhi na mahitaji yake ya ziada kama msichana na matokeo yake binti atanunuliwa taulo za kike na watu wa nje mwisho analeta mimba nyumbani anakuja kuongeza mzigo nyumbani.

Na mwisho Diwani huyo ameongezea kwa kukipongeza kituo Cha Taarifa na Maarifa kata ya Mabwepande kwa kushirikiana na shirika la TGNP kwa kutoa elimu hiyo kwa wajasiriamali kwani itawasaidia wafanyabiashara wa soko hilo kuweza kujisimamia wenyewe katika biashara zao ili waweze kuona faida na kuweza kukuza mitaji yao kama wajasiriamali.
Muwakilishi wa kituo Cha Taarifa na Maarifa kata ya Mabwepande  Farida Seif, akifafanua jambo katika semina ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wa soko la Bunju "B"
Kwa upande wake muwakilishi wa kituo Cha Taarifa na Maarifa Mabwepande  Farida Seif amesema kuwa hii ni awamu ya pili ya mafunzo ambapo mwanzo walianza kutoa mafunzo katika soko la mji mpya na leo wamekuja katika soko la bunju "B", lengo likiwa ni kuwawezesha wajasiriamali kuweza kujipatia kipato cha ziada kupitia rasilimali zinazowazunguka.

Ameongeza kuwa KC Mabwepande tumekuja leo kuwafundisha wajasiriamali wa soko la Bunju "B" jinsi ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na namna ya kutengeneza pilipili kwa ajili ya chakula, Na hii ikiwa ni sehemu ya mrejesho wa mafunzo tuliyopewa na TGNP kwa ufadhili wa COADY Institute. 
Mfanyabiashara wa soko la Bunju "B" Josephine Michael akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo katika semina iliyofanyika sokoni hapo.
Naye mmoja wa  wajasiriamali wa soko hilo Bi. Josephine Michael Amewashukuru TGNP kwa kupitia kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Mabwepande kwa kuweza kuwaletea elimu nzuri yenye kuwajenga na kuwapa mbinu mbalimbali za kujiogezea kipato.

Ameendelea kusema kuwa yeye Kama yeye amejifunza kuwa hata mzazi wa kiume anayo Haki ya kujua mzunguko wa siku za binti yake ili aweze kumtengea bajeti ya taulo zake za kujistili wakati wa hedhi ili kuepusha changamoto za binti kutafuta huko nje.

Na mwisho ameongeza kwa kuwashukuru viongozi wao wa kata pamoja na kituo cha Taarifa na Maarifa Mabwepande kwani kimekuwa sauti ya wananchi wanyonge kwa kuweza kuwaelimisha namna ya kupata mikopo ya halmashauri pamoja na kudai Haki zao za msingi kwa serikali na hata Jamii kwa ujumla.
Mfanyabiahara wa soko la Bunju "B" Ally Said Kagoma akichangia mada katika semina ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wa soko hilo.
Shughuli zikiendea sokoni Bunju "B"
Somo la utengenezaji wa Pilipili likiendelea.
Baadhi ya wajasiriamali wakionja pilipili wakati mafunzo yakiendelea katika soko la Bunju "B"
Baadhi ya wajasiriamali wa soko la Bunju "B" wakifuatilia mafunzo kwa umakini.


Muwakilishi wa Shilika la TGNP Hans Obote akiendelea kutoa elimu ya jinsia kwa wafanyabiashara wa soko la Bunju "B".

Hakuna maoni