BASATA Kufanya Mkutano wake Mkuu Septemba 29 Dar
Na Mussa Augustune.
Baraza la Sanaa Nchini (BASATA) limeandaa mkutano mkuu wa Mwaka utakaofanyika Septemba 29 mwaka huu utakaowezesha kuwakutanisha wadau wa sanaa kujadiliana njia bora za kuboresha sekta ya Sanaa kuwa biashara.
Akizungumza na wanahabari Kaimu Mtendaji wa Basata Matiko S.Mniko amesema kwamba mkutano huo una kauli mbiu ya " Sanaa Biashara" kutokana na serikali kuazimia kuifanya sekta ya sanaa kua rasmi ili sekta hiyo iweze kua sekta ya biashara na kua chanzo cha kipato kwa wadau wa sanaa,pia kulipatia kipato Taifa.
Aidha amesema kwamba sanaa imekua na mchango mkubwa wa kuongeza ajira na pato la Taifa nakwamba serikali imetenga kiasi cha fedha shilingi bilioni 1.5 ili kutoa elimu na mikopo ya gharama nafuu kwa wadau wa sekta ya sanaa ili kuifanya sanaa iwe biashara na sio burudani pekee.
" Tunataka kubadilisha fikra na
mtazamo kwa wadau wa sanaa watambue kwamba sanaa sio burudani tu bali ni
biashara,hivyo kupitia mkutano huu tutajadili namna yakuondoa changamoto ili
kuifanya sekta ya sanaa kua ya biashara" amesema Bw.Matiko.
Kwa upande wake Raisi wa shirikisho la Muziki Mwimbaji nguli wa muziki wa taarabu, Mzee Yusuph amesema kwamba mkutano huo utawasaidia wasanii kujibu mahitaji yao kutokana na kupata nafasi ya kutoa maoni yao ya kuboresha sekta ya muziki.
"Hii siku itatusaidia kufahamu wapi twende tukapate haki zetu pindi tunapopatwa na changamoto katika kazi zetu,kwahiyo majukwaa kama haya yanatusaidia kujadili yote tunayohitaji ili muziki wetu uzidi kukua na kua biashara,nawaomba wasanii wajitokeze kwa wingi siku hiyo" amesema.
Bw.Elia Mjata ambae ni rais wa shirikisho la filamu Nchini ameipongeza BASATA kuwashirikisha katika mkutano huo nakwamba ndoto yao ambayo walitamani filamu kutambulika kua biashara imeanza kuonekana hivyo amewataka wasanii wa filamu wajitokeze kuiuunga mkono serikali katika kuirasmisha sanaa kua biashara.
" Filamu ni biashara tunaishukuru Basata kwa kutushirikisha,sisi toka awali tulijua sanaa ni biashara kumbe na Basata wanasema sanaa ni biashara sasa tuanaongea lugha moja hivyo naamini tutafanikiwa katika kuifanya sekta hii kua ni biashara" amesema.
Nae raisi wa shirikisho la sanaa za Maonyesho Tanzania Bi .Cynthia Henjewele amesema mkutano huo utakau na tija kubwa kwani umelenga kujadiliana mambo muhimu yanayoikumba sekta ya sanaa ikiwemo sanaa ya maonyesho nakuifanya sanaa kua biashara,nakuwataka wadau wa sanaa wajitokeze kwa wingi katika mkutano huo.
Kwa upande wake rais wa shirikisho la sanaa za ufundi Nchini Adrian Nyangamalle amesema kwamba mutano huo utawasaidia kujadiliana mambo nakuwafanya watu wajue kwamba sanaa sio anasa ni burudani na nibiashara.
"Mfano Mamlaka ya Mapato Nchini
(TRA) wamekua wakitoza kodi kubwa kwa vifaa vya sanaa kwasababu wanadhani
vyombo vya sanaa ni anasa,hivyo tutajadiliana ili kuwafanya wadau
mbalimbali wajue kua sanaa sio anasa bali ni burudani na nibiashara
amesema Nyangamalle.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni