WANASEMINA ZA GDSS WAFANYA UCHAMBUZI WA TAARIFA YA MAPATO KATIKA SEKTA YA MADINI.
Baadhi ya sheria zetu za madini zinahitajika kufanyiwa maboresho kama siyo kusukwa upya kwani zimekuwa zikiwanufaisha sana wawekezaji ambao wengi ni wageni kuliko wazawa.
Afisa Programu Mwandami wa TGNP. Joyce Mkina akiwaongoza wanajamii kujadili sekta ya madini nchini. |
Hayo yameelezwa
mapema jana Septemba 22, 2021 na Afisa programu mwandami wa TGNP Bi. Joyce Mkina katika semina za Jinsia na Maendeleo
(GDSS), ambapo ameshirikiana na wanajamii kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar
es salaam kufanya uchambuzi wa taarifa za Mapato kupitia Sekta ya Madini.
Amesema kuwa
sheria hii kuna baadhi ya vipengele vimeshindwa kumuwajibisha muwekezaji moja
kwa moja, kwa mfano kipengele kinachosema muwekezaji anapaswa kuboresha makazi
au kuanzisha makazi mapya kwa wale anaotaka kuwaondoa katika eneo husika sheria
haijasema ni kwa muda gani anapaswa kufanya hivyo.
“Sheria hii haitoi
ufafanuzi wa moja kwa moja inaposema kuboresha makazi bila kumpa muda maalum na
ndio inakuja kuwa mtu amekaa miaka kadhaa anakwambia ajapata chochote kama
hakupata sasa miaka yote hiyo alikaa kufanya nini, na inatokea mpaka anaondoka
bila kufanya chochote na kampuni inabadilishwa jina huu ndio mchezo wanaotuchezeaga
hawa wawekezaji” Amesema Joyce
Kwa upande
wake Mtenganda Hosein mkazi wa kata ya Mabibo amesema kwa yeye angependa sheria
hii ingweza kuwakutanisha wahusika moja kwa moja kujadiliana kati ya mwenye
eneo na muwekezaji ili waweze kufanyiana tathmini ya kiwango sahihi cha
kulipana.
Naye Rhoda Mdoe
mkazi wa Mburahati ameitaka serikali na taasisi binafsi kuweza kupeleka elimu
kwa wakazi wa maeneo ya karibu na migodi kwani hii itaweza kuwasaida kufahamu
haki na madai yao kwa muwekezaji.
Mmoja wa
wachangiaj Bw. Kennedy Macher amsema kwa upande wake ameona ingependeza Zaidi kwa
yule ambae eneo lake litabainika kuwa na madini basin a yeye apewe hisa katika
kampuni hiyo itakayokuwa ikichimba madini hayo.
Na mwisho angetamani
pia kuona wakazi wanaoishi karibu au kuuzunguka mgodi huo kupewa nafasi ya
kwanza katika kupatiwa ajira kwani hii itasaidia wakazi wa eneo husika
kunufaika na uwepo wa mgodi huo.
Afisa Programu Mwandami wa TGNP. Joyce Mkina akitoa ufafanuzi wa jambo fulani, mbele ya wanajamii ambao hawapo pichani. |
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo kwa umakini. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni