Taasisi Za Dini Hazihusiki Zoezi La Kuhuisha Daftari La Usajili
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene amesisitiza jamii kutambua kuwa suala la kuhuisha daftari la usajili wa Taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya wizara hiyo halitahusisha Taasisi za kidini ili kuziwezesha kufanya kazi kwa uhuru na utulivu na kutoa mchango wao kwa Serikali lengo likiwa ni kuwaletea watanzania maendeleo.
Simbachawene alisema hayo jana wakati akitoa salamu za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sherehe za kusimikwa kwa Askofu wa jimbo Katoliki Morogoro Lazarus Msimbe zilizofanyika katika viwanja vya seminari ya Mtakatifu Peter mjini hapa ambapo alisema kuhuishwa kwa usajili wa daftari hilo hakutahusisha taasisi za kidini ili kuwapisha kufanya shughuli zao
Alisema zipo jumuiya za sekta binafsi na za kidini na kwamba uhakiki huo utafanywa kwenye jumuiya nyingine za binafsi zote na sio za madhehebu ya dini wala Taasisi za madhehebu hayo.
Waziri huyo alisema anaimani na Askofu Msimbe ambaye anaweza kukabiliana na wakristo wa mitandao waliopo kwa sasa.
“bahati mbaya sana baba askofu unalichukua kanisa la Morogoro kama yalivyo makanisa mengine duniani na Tanzania ni wakati wa wakristo wa dotcom, wa whatsapp, utube, na wa mitandao, wakristo wa tofauti kidogo lakini Imani yangu ni kwamba kanisa la Mungu kupitia kwako hapa Morogoro litapiga hatua kubwa” alisema.
Alisema idadi ya watu kubwa waliofika eneo hili kwenye kusimikwa kwao inaashiria wa Imani nawe kubwa huku ikionesha kuwa watakupa ushirikiano wa kutosha.
Akiendesha ibada ya kumuweka wakfu na kumsimika Askofu Msimbe, Askofu Mkuu Kiongozi na Balozi wa Papa nchini Tanzania Mareck Solczynski amewataka wakristo kumpokea Askofu Msimbe kama mjumbe wa Mungu na jukumu la kuwaongoza kuelekea ufalme wa Mungu kwa sababu hata watu walishindwa kuwa na Imani na Yesu na kumfanya kutokuwa na nguvu wakati mwingine.
Alisema Askofu ni jina linalomaanisha utumishi wala si alama na kwamba jina hilo linalopaswa kutumikia na sio kutawala kwa sababu kadiri ya agizo la mwalimu wao ni kwamba aliye
Hakuna maoni
Chapisha Maoni