Zinazobamba

Jaji Mutungi ataja ratiba ya kukutana na wadau wa siasa

Na Mussa Augustine.

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini inatarajia  kukutana na wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa ikiwemo Jeshi la Polisi  kwa lengo la kufanya  majadiliano ya kutafuta  suhulu  kutokana na mvutano ambao umekuwa ukitokea kati ya vyama vya siasa na Jeshi la Polisi Nchini.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amesema nia ya vikao hivyo  ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya  vyama Siasa.

 

Jaji Mtungi amesema kikao cha kwanza Cha wadau kitafanyika Septemba 23 mwaka huu ambapo ofisi hiyo itakutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

 

Aidha  Jaji Mutungi amesema kwamba Septemba 30 ofisi hiyo itaitisha kikao cha kamati ya Uongozi ya vyama vya Siasa ambapo kikao hicho kitaongozwa na kanuni ya baraza la vyama vya Siasa kwa ajili ya kuandaa agenda zitakazotumika katika mkutano huo wa wadau wa siasa.

 

PIA amesema kuwa Octoba 13 mwaka huu baraza la vyama siasa litafanya mkutano mkubwa visiwani Zanzibar ambapo utashirikisha wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa.

 

"Mkutano huu utaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye anamafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya Siasa kuelezea chagamoto zinazowakaba na kufikia Maridhiano"amesema

 

Vikao hivi vinakuja ikiwa bado kunamalalamiko ya baadhi ya  wadau wa vyama vya Siasa kushidwa kufanya mikutano yao kwa kueleza Jeshi la Polisi kuwaingilia. 

Hakuna maoni