Zinazobamba

BBF YAIOMBA JAMII KUJENGA UTARATIBU WA KUCHANGIA DAMU

Na Fatma Ally, Dar es Salaam

Jamii imeshauriwa  kujenga tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili kuwasaidia watu wenye mahitaji ya kuongezewa damu ikiwemo mama wajawazito, wagonjwa wa Sikoseli, Kansa,Haemophilia pamoja na watoto chini ya miaka mitano.
Wakazi mbalimbali wa mkoani Dar es salaam wakijitolea kutoa damu kwa hiari.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Shirika liliso la Kiserikali linalojihusisha na uhamasishaji wa uchangiaji damu, Bone and Blood Foundation (BBF) Neema Mohamed wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, katika kuhakikisha jamii inajenga utamaduni wa kuchangia damu kwa lengo la Shirika lisilo la BBF kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu salama (NBTS)
wametoa elimu kwa wakazi mbalimbali wa jiji hilo juu ya  umuhimu wa kuchangia damu.

Amesema kuwa, katika kuhakikisha huduma ya damu inapatikana kwa wakati BBF imekuwa ikitoa elimu ya uchangiaji damu ambao utasaidia kuondokana na vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu.

"Tumekuwa tukitoa elimu mara kwa mara kwa jamii ili iweze kutambua umuhimu wa kuchangia damu tumetambua kuwa kikwazo kikubwa kinachosababisha watu kushidwa kuchagia damu nikutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha"amesema Neema.

Aidha, amesema kuwa  BBF wamejipanga kufika maeneo mengi zaidi nchini ambapo wataanza  katika Wilaya Ilala, Kinondoni na Temeke kwa lengo la kuendelea kuelimisha jamii juu ya umuhumu wa kuchangia damu.

Hata hivyo, amesema kila ifikapo
Septemba huwa  ni mwezi wa kujenga  uelewa juu ya ugonjwa wa sikoseli kutokana na wagonjwa hao kutengemea damu kama tiba.

Aidha, amelipongeza Shirika la SICKLE CHARTA kwa kuifadhili program hiyo, ambayo imekuwa ikitoa elimu juu ya uhamasishaji wa watu kuchangia damu ambapo zoezi  hilo limetoa mwamko mkubwa jamii kuhusu watu kuchangia damu.

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa BBF Nobert Silayo amesema uchangiaji wa damu ni muhimu kwa jamii kwani watu wenye uhitaji wa kuongezewa damu wamekua wakiongezeka siku hadi siku, hivyo ni vyema jamii kuweka kipaumbele kwa kutoa damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu.

Amesema kuwa endapo jamii itajenga utamaduni wa kuchagia damu mara mara itasaidia kwa kiwango kikubwa kunusuru maisha ya watu wengine ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa damu.

Naye, Afisa Mahusiano wa Bone and Blood Foundation, (BFF) Bora Hilary amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

"Tunaomba jamiii ijitokeze kwa wingi kuchangia damu,unapochangia Leo unaokoa maisha ya watu wenye uhitaji, mahitaji ya damu kwa watu yamekua makubwa hivyo, tunaomba jamii iekeze kwa kuokoa maisha ya wengine"amesema Bora.

 Jackline Yahaya mkazi Tabata kisiwani ambae alichangia damu katika zoezi hilo amesema damu ni muhimu kwa jamii nzima kwani uhitaji wa damu unawagusa watu wa aina mbalimbali, hivyo ni vyema kila akaweza kushiriki kuchangia damu.
 
Ramadhani Juma ni mkazi wa Mazense amesema amekuwa akichagia damu mara kwa mara na kutoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu huo kwani damu ni muhimu kwa maisha ya watu.
Jackline Yahaya mkazi wa tabata akitoa damu kwa hiari, mapema jana siku ya Simba Day uwanja wa Taifa mkoani Dar es salaam.

Mkazi wa Manzese mkoani Dar es salaam ambaye pia ni shabiki wa timu ya Simba Bw. Ramadhani Sadiki akipima virusi vya Ukimwi kabla ya zoezi la kujitolea damu kwa hiari.

Katibu wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na uhamasishaji wa uchangiaji damu, Bone and Blood foundation (BBF) Neema Mohamed akichukua maelezo kwa mwananchi kabla ya kuchangia damu.

Zoezi la uchangiaji wa damu Kwa hiari likiendelea mapema jana uwanja wa Taifa mkoani Dar es salaam, ikiwa ni siku ya Simba Day.
Viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Bone and Blood foundation (BBF) wakiwa katika picha ya pamoja.

Hakuna maoni