Dar Boxing Derby kufanyika Kines Octoba 30, kiingilio Buku 7 tu
Kwa mujibu wa Promota wa Pambano hilo, Captein
Suleiman Semunyu, amesema viingilio hivyo vimepangwa na mashabiki wa mchezo huo
na kwamba ameona akubaliane nao ili kuenenza burudani kwa umma.
Amesema kwa mara ya kwanza pambano hilo litapigwa
katika viwanja vya wazi na kwamba mashabiki wamechagua uwanja wa mpira wa Kinesi
ndio uwe sehehmu sahihi ya mchezo.
Amekubali ombi lao huku naye akipenyeza ombi lake la
kuwataka mashabiki wa mchezo huo kujitookeza kwa wingi siku ya tukio kupata
burudani.
Mabondia Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ dhidi ya
Adam Kipenga watauwasha moto siku hiyo ambayo imepewa jina la Mwana ukome baada
ya kuzinduliwa Ijumaa iliyopita kwenye Uwanja wa Las Vegas uliopo
Mabibo, Dar.
Huu ni msimu
wa pili kufanyika kwa pambano la Dar Boxing Derby ambapo pia Idd Pialali
atapanda ulingoni dhidi ya Ramadhan Shauri wakati Seleman Kidunda akipanda
ulingoni kuzichapa na Jacob Maganga wa Tanga huku Ismail Galiatano akitarajia
kumaliza utata na Allan Kamote na Haji Juma akimaliza na George Bonabucha.
Wengine ni Hassan Ndonga dhidi ya James Kibazange,
Grace Mwakamele na Happy Daud Halima Vunjabei mpinzani wake anatarajia kuwekwa
wazi wakiwemo mabondia wengine watakaopanda ulingoni.
Akizungumza katika uzinduzi huo, promota wa pambano
hilo, Kapteni Seleman Semunyu alisema kuwa awali pambano hilo lilipangwa
kufanyika kwenye Ufukwe wa Kidimbwi lakini kutokana na maombi ya mashabiki
wengi sasa litapigwa kwenye Uwanja wa Kinesi Dar.
“Dar Boxing Derby ambayo itaenda kwa jina la. Mwana
Ukome litapigwa hapa Kinesi badala ya Kidimbwi kutokana na maombi ya wadau
wengi ambao wakati wote wamekuwa wakitupa sapoti kubwa katika mapambano
yetu.
“Niwaambia tu kwamba Chichi Mawe na Kipenga,
Ramadhan Shauri na Idd Pialali, Bonny Sela na Sadick Momba lakini Seleman
Kidunda na Jacob Mangaga, Allan Kamote na Ismail Galiatano, George Bonabucha
akitarajia kucheza na Haji Juma hii ni kwa ajili ya wadau wangu ambao wamekuwa
sapoti kubwa kwetu Peak Time Media katika kazi zetu,” alisema Kepteni Semunyu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni