Miss Kanda ya Mashariki kuondoka na million 2 pamoja na crown
Maandalizi ya Shindano
la Miss Tanzania Eastern Zone yamekamilika, kilichobaki ni kumtambua nani
ataibuka kidedea na kujinyakulia zawadi nono hiyo septemba 24 huko mkoani
Morogoro.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya Tips Forum, Mhandisi Nancy Matta amesema
mbali ya kuibuka na zawadi mshindi pia atapata fursa ya kuwakilisha katika
mashindano ya kitaifa ya Miss Tanzania.
Alisema mpaka
wanafika kuwashindanisha katika ngazi ya kanda, tayari washiriki mbalimbali
walishindana kuanzia ngazi ya mkoa.
Alisema mwaka huu
wamejipanga vizuri zaidi kuhakikisha shindano hilo linakuwa la kipekee zaidi
ili kupata mshindi ambae anaweza kunyakua taji la Miss Tanzania na kuiwakilisha
nchi vizuri
"Mashindano ya
mwaka huu yanatarajiwa kufanyika katika hoteli ya Morena ambapo mshindi wa
kwanza atapata kitita cha shilingi milioni 2, mshindi wa pili sh milioni
1.5 na mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha sh milioni 1"
Aidha Mhandisi Nancy
aliongeza kuwa lengo kubwa la shindano hilo ni kukuza sekta ya urembo na
kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake moja
ya wadhamini wa shindano hilo Bodi ya Taifa ya utaliii (TTB), BI Maria Mafie
alisema wameamua kudhamini mashindano hayo ya ulimbwende ili kuweza
kukuza na kutangaza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.
Nae afisa masoko
hoteli ya Dynasty Beach ambayo washiriki wa kinyanganyiro hicho wameweka kambi
Bw. Charles alisema wataendelea kuunga mkono mashindano hayo na ana imani
mshindi ataweza pia kuibuka na taji katika mashindano ya Miss Tanzania.
Kwa upande wake
Meneja mauzo wa hoteli ya Serena Bw. Shaban Kaluse alisema kuwa wameamua
kuwa sehemu ya wadhini wa mashindano hayo wakiamini kuwa yatakuwa chachu ya
kuutangaza utalii wa Tanzania.
Miss Tanzania
Eastern Zone ldhaminiwa na makampuni mbali mbali ambapo mdhamini mkuu
mwaka huu ni chanel ya Utalii ya Taifa (Tanzania Safari Channel) ya
shirika la utangazaji Tanzania (TBC).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni