Zinazobamba

Stive Nyerere - Watanzania jitokezeni kuchanja kwa hiari chanjo ya Uviko 19.

Na Mussa Augustine.

Taasisi ya Wazalendo kwanza inatoa hamasa kwa  Watanzania kujitokeza kwa hiari kupata chanjo ya uviko 19 nakuachana na upotoshaji unaoenezwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa  kupitia mitandao ya kijamii kuwa  chanjo hiyo ina madhara kwa binadamu.
Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa taasisi hiyo Stive Mengele maarufu kama Stive Nyerere ambaye pia ni balozi wa Wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es saalam, nakusema kuwa  Kuna baadhi ya wanasiasa wamekua wakiwashawishi Watanzania kupitia mitandao ya kijamii wasiende kuchanjwa kwa hiari hali mabayo inasababisha kupoteza uzalendo katika kukabiliana na janga hilo.

" Wapo wanaotumika kisiasa kuhimiza wenzao wasichanje ,kama wewe hauchanji acha watu watumie Uhuru wao wa kuchanja au kutokuchanja ,sisi Wazalendo kwanza tumechanja tunahimiza wale wanaowashawishi Watanzania wasichanje kwa hiari yao waacha tabia hiyo" alisema Stive Nyerere.

Nakupongeza kwamba " tusitumie mitandao yetu ya kijamii kupotosha Jamii ,mataifa yaliyoendelea yanatumia mitandao ya kijamii kutangaza Mambo  muhimu kwa taifa lao ikiwemo Sera za Uchumi.

 Aidha alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kama Amiri Jeshi Mkuu hivi karibuni alijitokeza kuonyesha uzalendo wa kuchanja, hivyo Watanzania wakiwemo vijana na viongozi mbalimbali wajitokeze kwa hiari kuchanjwa ili wajiweke salama kwa afya zao.

Kwa upande wake msanii wa uigizaji  Abdalah Mkumbila maarufu kama Mhogo mchungu aliwashauri Watanzania kuendelea kuchukua hatua za tahadhari kwani Ugonjwa wa Uviko 19 upo nakwamba kundi la watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 ndilo lipo katika hatari zaidi .

" Jitetee mwenyewe kwanza halafu na watu wakutetee,tunaomba Watanzania mjitokeze kwa hiari kupata chanjo ,ili taifa liwe na maendeleo lazima wananchi wake wawe wazima" alisema Mhogo Mchungu.

Taasisi ya Wazalendo kwanza imekua mstari wa mbele katika kuhimiza Watanzania hususani vijana kuwa wazalendo katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Hakuna maoni