TIC- Hali ya Uwekezaji Nchini imepanda licha yakuwepo kwa ugonjwa wa Covid 19.
Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Nchini( TIC) Dr.Maduhu Kazi amesema hali ya uwekezaji hapa nchini imepanda ambapo kati ya miradi 235 iliyosajiliwa na kituo hicho asilimia 56 ya miradi hiyo inawahusisha Watanzania katika umiliki wake.Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Nchini( TIC) Dr.Maduhu Kazi. |
Alifafanua kwamba katika kipindi cha mwaka wa 2020/2021 idadi ya miradi ya wawekezaji ya watanzania pekee iliyosajiriwa ni 66 sawa na asilimia 28 ya miradi yote 235 iliyosajiliwa kwa kipindi hicho , huku miradi ya ubia kati ya watanzania na wageni iliyosajiliwa ni 65 sawa na asilimia 28 ya miradi yote iliyosajiriwa.
"Tic imeendelea kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi nchini sambamba ba uwekezaji nje ya nchi ambapo jitihada zimefanyika kutafuta wafadhili kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ambayo inatoa mikopo nafuu ili kuwezesha uwekezaji ." alisema.
Alisema kwamba taarifa ya uwekezaji Kidunia 2020 ( world investment Report 2020 ) iliyotolewa na UNCTAD inaonyesha kwamba upande wa nchi za jumuia ya Afrika Mashariki , Tanzania imepata uwekezaji mkubwa wa dola za kimarekani Bilioni 1.ukilinganisha na nchi nyingine za Burundi kwa dola milioni 6, Kenya Dola milioni 717, Rwanda Milioni 135 na Uganda milioni 823 ,
"Changamoto ya Uviko 19 imesababisha Tanzania kuvutia mitaji ya viwanda vya madawa ya binadamu hususani PPE , " alisema Dr.Maduhu Kazi.
Aidha aliendelea kusema kuwa Tic inampango wa kutekeleza malengo yake ya baadae ikiwemo kushirikiana na wadau wa ndani wakiwemo wa sekta binafsi na nje ya nchi, pamoja na kutangaza miradi mbalimbali ya uwekezaji.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni