Zinazobamba

KAWASO - yaomba Ushirikiano kwa mamlaka za serikali.

Na Mussa Augustine.

Chama Cha Wamachinga Kariakoo (KAWASO) kimeziomba Mamlaka za serikali zinazohusika na masuala ya Biashara kushirikiana kwa pamoja na wafanyabiashara wadogo(Wamachinga) ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili na kuwafanya wainuke kibiashara.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wamachinga Kariakoo (KAWASO) Namoto Yusuph Namoto akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo mkoani Dar es salaa.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Namoto Yusuph Namoto wakati akifanya mahojiano Maalumu na kituo hiki ambapo amebainisha kuwa Mamlaka za Biashara hazina ofisi maeneo ya soko hilo hali ambayo inachangia Wamachinga kudolora kibiashara.

Amezitaja baadhi ya Mamlaka hizo kuwa Ni pamoja na Shirika la viwango nchini ( TBS), Mamlaka ya Mapato (TRA), (FCC ),Mamlaka ya usajiri wa Biashara (BRELA) pamoja na maafisa wa Biashara na Miundombinu nakwamba Mamlaka hizo zingekuwepo karibu zingesaidia kutoa elimu kwa ukaribu kwa Wafanyabiashara.

" Hapa kariakoo kuna bidhaa mbalimbali zinazouzwa ambapo zingine ni feki lakini baadhi ya Wafanyabiashara hawana uwelewa wa kutosha namna ya kuzitambua bidhaa hizo,hivyo uwepo wa Taasisi hizi katika maeneo ya soko utasaidia Wafanyabiashara wadogo kuwa na uwelewa wakutosha wa namna ya taasisi hizo zinavyofanya kazi." alisema Namoto.
Akizungumzia kuhusu ugawaji  wa vizimba vya Biashara katika soko la Kariakoo kwa Wahanga wa ajali ya Moto uliotokea hivi karibuni na kuunguza maeneo ya soko hilo Namoto amesema kwamba mpaka Sasa jumla ya Wafanyabiashara wapatao 560 tayari wameshapatiwa  wamepatiwa  maeneo ya kufanyia kazi pamoja na meza za biashara.
  
Amesema kwamba jumla ya Wahanga 780 wanatarajiwa kupatiwa maeneo ya kufanyia Biashara ambao kwa sasa 560 tayari,ambapo Wahanga  waliobaki meza zao zinaendelea kutengenezwa nakutumia fursa hiyo kuwaomba wawe wavumilivu kwani zoezi hili linafanyika kwa awamu

Aidha pia aliwaomba Wafanyabiashara wadogo( Wamachinga) kujitokeza kuchukua vitambulisho vya ujasiliamari ili waweze kupata fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya Biashara kutoka Taasisi za kifedha kwani vitambulisho hivyo vimekidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo.

Hata hivyo aliwataka Wafanyabiashara hao waendelee kuchukua tahadhali ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ungonjwa wa uviko 19 Kama miongozo inavyoelekeza ikiwa ni kuvaa barakoa, kunawa mikono pamoja na kutakasa mikono yao.

Hakuna maoni