Zinazobamba

TIC , ZIPA zatiliana saini ya mashirikiano kukuza sekta ya uwekezaji.




Na Mussa Augustine.

Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimetiliana saini ya mashirikiano na Mamlaka ya Ukuzaji Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa ajili ya kutekeleza maeneo kumi na mbili muhimu katika sekta ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Dr. Maduhu Kazi wa upande wa kushoto, na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukuzaji Uwekezaji Zanzibar ( ZIPA) Shariff Shariff wakisaini mkataba wa Makubaliano wa kukuza sekta ya uwekezaji upande wa Tanzania bara na Zanzibar.

Akizungumza jijini Dar es salaam baada ya kutiliana saini, Mkurugenzi Mtendaji wa  kituo hicho Dr. Maduhu Kazi amesema malengo ya makubaliano hayo ni kukuza sekta ya uwekezaji upande wa Tanzania bara na Zanzibar.

Aidha Dr.Kazi amesema maeneo ambayo yamepewa msukumo mkubwa katika mashauriano hayo ni pamoja na kufanya utafiti vyanzo vya uwekezaji pamoja na kubadilishana taarifa na uzoefu na ujuzi kwa wafanyakazi wa taasisi hizo.

Maeneo mengine ni kutangaza vivutio vya uwekezaji kwa pamoja ,pia kushirikiana kwenye maonyesho yanayohusu masuala ya uwekezaji huku akisisitiza kwamba masuala ya kimufumo ( tehama) kuhusisha pande zote mbili ( Tanzania bara na Zanzibar) tayari wataalamu wameanza kuyafanyia kazi.

" Tutashirikiana vizuri na ZIPA katika maeneo mbalimbali, mfano masuala yakutangaza vivutio vya uwekezaji pamoja na kuandaa kwa pamoja maonyesho ya uwekezaji ,kufanya tafiti mbalimbali za kutangaza na kuvutia  wawekezaji , lakini eneo jingine muhimu ni kubadilishana uzoefu na ujuzi kwa watumishi wetu " alisema Dr Kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na TIC inaonyesha kuwa hali ya uwekezaji nchini  Tanzania inazidi kupanda nakushika nafasi ya kwanza kwa nchi za Jumuiya ya afrika mashariki  licha ya kuwepo kwa ugonjwa wa uviko 19 , hivyo kufuatia hali hiyo mashirikiano hayo ya ZIPA na TIC yataongeza zaidi idadi ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukuzaji Uwekezaji Zanzibar ( ZIPA) Shariff Shariff amesema kwamba kupitia mashirikiano hayo itasaidia kupiga hatua kubwa yakutangaza vivutio vya uwekezaji ili kukuza sekta hiyo.

" Mashirikiano haya yanaleta mafanikio makubwa sana , hivyo ZIPA na TIC tutahakikisha tunafanya kazi hizi kwa pamoja ili kufikia malengo yetu alisema Shariff.

Nakuongeza kwamba " Kinachonifurahisha zaidi haya mashirikiano yamebarikiwa na wakuu wa nchi ,tutashirikiana vizuri katika kutekeleza mambo muhimu yakukuza sekta ya uwekezaji kwa kutangaza vivutio vya uwekezaji vya vya Tanzania bara na Visiwani Zanzibar" alisema.

Hakuna maoni