Kamisaa Anne Makinda awasisitiza wadau kuihamasisha na kuielimisha jamii umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi wa Tanzania Bara ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda amewasisitiza Wadau washiriki wa Mkutano wa kujadili Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Mwezi Agosti mwakani kutoa maoni na mapendekezo yatakayochangia uboreshaji wa mkakati huo pamoja na kuituma fursa hiyo kuipa jamii uelewa na umuhimu wa sensa hiyo kitaifa.
Msisiitizo huo ameutoa leo
jjijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano huo ulioshirikisha wadau
mbalimbali wakiwemo wanahabari, wahariri wa vyombo vya habari, Jukwaa la Habari
Tanzania (TEF), taasisi za kitakwimu, Viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) pamoja na wa Ofisi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar (OCGS).
Amesema kuwa Tanzania ina watu
zaidi ya milioni 60 na kwamba wadau washiriki wanatakiwa kutambua umuhimu kwa
taifa kwa kuwa wazalendo baada kuchangia maboresho ya mkakati huo kwenda
kuelimisha jamii umuhimu wa sensa hiyo itakayofanyika nchi nzima.
" Nwawaomba mtumie usukani
huu kwenda kutoa elimu kwa jamii juu umuhimu wa sensa baada ya majadiliano kila
mshiriki mdau awe mzalendo ajitoe kwenye kuelimisha na kuboresha mkakati
huo," amesema Kamisaa Makinda.
Amebainisha kuwa kila baada ya
miaka 10 nchi hufanya sensa hiyo ambapo idadi ya watu huhesabiwa kwa kuuliza
maswali sawa kwa kila mwananchi na kwamba huisaidia Serikali kupata taarifa
muhimu za kupanga maendeleo inayoendana na jamii pamoja na kuzisaidia Serikali
za Mitaa, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kupima na kutekeleza mipango
hiyo.
Amessisitiza kuwa senya ya mwaka
2022 itaegemea kuuliza maswali katika vipengele mbalimbali vikwemo vya
umri, jinsi, ndoa, uraia, uhamiaji, vitabulisho vya taifa, uhai wa wazazi, vifo
vya uzazi kwa wanawake na hali ya ajira.
Vingine ni hali ya elimu,
umiliki wa ardhi, udhibiti wa Mazingira, taarifa za kilimo, misitu, Mfufo wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) pamoja na umiliki wa majengo.
Ameongeza kuwa sensa ya mwakani
itakuwa sensa ya sita tangu kuundwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzyika kufanyika
na kwamba sensa ya majaribio itafnyika mwishoni mwa mwezi wa Agosti mwaka huu.
Amefafanua kuwa dhamira ya
Serikali zote ni kufanya sensa iliyo bora tofauti na zilizopita kwani
itafanywa kwa kutumia matumizi ya Tehama yatakayosaidia kupungua gharama,
kuokoa muda,makosa ya kibinadamu na utoaji takwimu sahihi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Takwimu za Kijamii kutoka OCGS, Khadija Khamis amesema wanatarajia
kufanya sensa kwa kuwa katika mchakato wa kuboresha mkakati huo wameshirkisha
wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, Serikali, na sasi za kiraia huku
akiongeza sensa ya majaribio visiwani humo itafanyika mwishoni mwamwezi huu
katika wilaya 10.
Aidha, amesema sensa ya watu na
makazi hutumika kupima na kupanga maendeleo ya jamii, sera, ajira na mahitaji
ya makundi mbalimbali kulingana kufuatana na jinsi pamoja na umri.
Naye Meneja Ofisi ya NBS wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Albert Kapala amesema kwa kushirikiana na wadau hao wapo
katika mkakati kabambe wa kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha kabla ya
kufanyika sensa hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni