"Vurugu huingilia haki za binadamu" Warioba
Katika
Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kituo Cha sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kimeadhimisha siku hii leo kwa kuhamasisha amani huku kauli
mbiu ikiwa ni "Haki ni Maendeleo, Simamia Haki".
Akizungumza katika hafla
hiyo iliyohudhuriwa na taasisi mbalimbali za kupinga ukatili, Jaji Mstaafu
Joseph Warioba, amesema kuwa vurugu huingilia haki za binadamu.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa LHRC,Anna Henga amewataka wanajamii kuacha kukaa kimya pindi
vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unapotokea.
Aidha, wamewataka wananchi
wote kuilinda amani ya nchi kwani amani isipoimarika kutatokea vurugu na
kushindwa kulinda haki za binadamu.

No comments
Post a Comment