Zinazobamba

SATA KUONGEZA WATAALAMU, ANGALAU KILA HOSPITALI YA MKOA KUNAKUWA NA DAKTARI BINGWA

Raisi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji na dawa za usingizi nchini (SATA) Dkt Mpoki Ulisubisya amesema wamejipanga kuboresha huduma na kuona ni namna gani wanaweza kutoa elimu ili kuongeza wataalamu
Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mapema leo hii alipokuwa akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa sita uliowakutanisha wataalamu wa kutoa huduma za dawa ya usingizi na ganzi wa ndani na nje ya nchi.
Profesa Mseru amesema kuwa wataalam wa kutoa dawa hizo kwa Tanzania wapo 40 ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu wataweza kufikia 50 baada ya wahitimu wa kazi hiyo kugradueti
“Bado kuna upungufu wa Wataalamu awali nchini kulikuwa na wataalam 10 na baadae wakaongezeka na kufikia 40 ila huitaji tunaitaji kufikia wataalam 200″amesema Profesa Mseru
Ameongeza kuwa, kwa sasa Serikali imeamua kusomesha zaidi ya wauguzi 100 ambao wataenda kutoa huduma katika hispital za rufaa na wilaya ili kukabiriana na cahagamoto.
Hata hivyo, amesema Tanzania kumekua na ongezeko la ajali za barabarani hivyo kupitia wataalam waliopo na watakao ongezeka watasaidia kuhuisha majeruhi mahututi na wanopoteza fahamu.
Kwa upande wake, Raisi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji na dawa za usingizi nchini (SATA) Dkt Mpoki Ulisubisya amesema lengo la mkutano huo ni kuweza kuboresha huduma na kuona ni namna gani wanaweza kutoa elimu ili kuongeza wataalam.
“Tutakuwa kuweka ushawishi kwa vijana kuweza kusomea ili kuongeza idadi yetu kwani kwa nchi nzima atufiki 50 ivyo tunataka tuwe wengi”amesema
Dkt Ulisubisya amesema lengo lao ni kuahikisha kila hospitali ya rufaa na mkoa inakua na angalau daktari bingwa mmoja.

Hakuna maoni