Zinazobamba

SERIKALI YA JPM YAENDELEA KUANGUKIA ''PUA'' MAHAKAMANI ,NI KWENYE KESI ZA UFISADI,SOMA HAPO KUJUA



NI wazi sasa ongezeko la Serikali ya Rais John Magufuli kushindwa mahakamani kwenye Kesi zinahusu ufisadi limezidi tamaradadi baada ya leo ALIYEKUWA mkurugenzi wa huduma za sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma ameachiwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Alikuwa  akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya milioni 323 kutoka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Esrow.

 Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa amemuachia huru Rugonzibwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kuomba kesi hiyo iondolewe mahakama chini ya kifungu cha 98 (a) cha  sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) na mahakama kuridhia.

Rugonzibwa alifikishwa mahakama kwa mara ya kwanza Januari 14,2015 na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru).

Akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya milioni 323  toka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Esrow.

Ambapo baadaye alibadilishiwa hati ya Mashtaka na kusomewa upya  ambapo hayakuonesha tena kuwa fedha zilizopokelewa na Mujunangoma toka kwa Rugemalira ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Kupitia hati hiyo mpya,  Rugonzibwa alikuwa akidaiwa kuwa Februari 5, 2014  akiwa mtumishi wa serikali kama Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipokea rushwa ya milioni 323 kupitia akaunti yake namba 00120102602001 iliyopo kwenye  benki ya  Mkombozi .

Alidaiwa kuwa alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa James Burchard Rugemalira, ambaye ni mshauri huru wa kitaalamu, mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo.

Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya kujipatia kiasi hicho cha fedha alishindwa kueleza maslahi yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara yake ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kwenye tume ya maadili  ya Viongozi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upelelezi  wa kesi hiyo ulikuwa umekwisha  kamilika.

Awali  Mujunangoma alikuwa akidaiwa kuwa  Februari 5, 2014 katika Benki ya Mkombozi iliyopo wilayani Ilala, Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokea rushwa ya  kiasi hicho cha fedha kutoka kwa James Burchard Rugemalira  kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo fedha ambazo ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.



Mshtakiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo,  kinyume na kifungu cha 15 (1)cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Namba 11 ya mwaka 2007 na alikuwa yupo nje kwa dhamana.