Zinazobamba

TECNO YAJA NA SIMU BOMBA KABISA,SOMA HAPO KUJUA


NA KAROLI VINSENT.
KATIKA kuhakikisha wanawasaidia watanzania kupata simu zenye kuwarahisishia mawasiliano katika kipindi hiki nchini inapokwenda kwenye uchumi wa Viwanda.
Kampuni ya simu inayofanya vizuri nchini ya TECNO imezindua simu mpya ya Tecno L9 plus ,ambapo wataaramu wanaitaja simu hiyo kufanya vizuri kwenye soko kutokana na kuja na ufumbuzi wa Tatizo la Chaji.
Akizingumzia simu hiyo Meneja Mauzo rejareja wa Kampuni ya Tecno,Moses Mtweve amesema lengo la Kampuni hiyo kuzindua simu hiyo ni kwa ajili ya kuwasaidia watanzania .
“Tecno L9 Puls itakuwa msaada mkubwa kwa watanzania na wateja wetu kwa ujumla ukizingatia kua umeme katika nchi yetu haujatengemaa kabisa kwa baaadhi ya mikoa kwahiyo watu wengi wanapata shida ya chaji,kwahiyo simu hii itawaondolea kadhia hiyo,”amesema Mtweve.
Mtweve ameongeza kuwa simu hiyo itaweza kukaa na chaji kwa saa 72  huku mtumiajia akifurahia huduma mbali mbali za mawasiliano.
“Simu ya Tecno kupitia L9 plus inawakikishia wateja kua watakaa saa 72 bila kuwaza lolote kuhusu chaji huku akiwa anafurahia huduma,ambapo hata chaji ikiisha ikichajiw akwa dakika tano mtumiajia ataweza kutumia kwa kupiga picha zaidi ya elfu moja  kwa chaji hiyo ya Dakika tano”ameongeza kusema Mtweve.
Mtweve pia, ametaja faidi nyingine kwa mtumiaji wa simu hiyo ni kufaudi picha kutokana na simu iyo kuwa na kamera ya nyuma na mbele pamoja kuwa tecnolojia ya usalama wa vidole.

Hata hivyo,Mtweve amewataka watanzania kujitokeza kwenye mawakala wa Tecno nchini kujipatia simu hiyo kwa bei nafuu.