Zinazobamba

LHRC YAMKALIA KOONI MAKONDA...YAPENDEKEZA RC MAKONDA KUPELEKWA JELA


Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dkt Kijo Bisimba akifafanua jambo kuhusu tukio la Makonda kuvamia ofisi za Clouds. Kulia ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) Bi
Ana Henga,

NA MWANDISHI WETU

Licha ya Rai wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuri  kutangaza hadharani juu ya hatma ya vitendo vya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda, kituo cha sheria na haki za binadamu kimeibuka na kutaka hatua zaidi kuchukuliwadhidi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Dkt.  Helen Kijo Bisimba amesema kitendo alichofanya Makonda hakipaswi kufumbiwa macho na kwamba wananchi wana uhuru kisheria kufungua kesi mahakamani kwa kuwa kitendo hicho kinavunja misingi iliyowekwa na katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

 Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam alidaiwa kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds kwa lengo la kushinikiza chombo hicho cha habari kurusha taarifa ambayo kituo hicho kiliona hakina sifa ya kwenda kwa mlaji. 

Taarifa hiyo ambayo ilitakiwa kurushwa kupitia kipindi cha The week end chart show ambacho kinaruka kila Ijumaa, ilishindika kwenda hewani baada ya kugundua kuwa ilikuwa ni ya upande mmoja.

DKT Hellen Kijo Bisimba akilaani vikali tukio hilo

Bi Helen Kijobi Simba alisema inafahamika kuwa kuna sheria kandamizi juu ya vyombo vya habari na hata muda mwingine hutishia kufungia vyombo hivyo. lakini hakuna sheria inayomtaka kiongozi yeyote kutumia chombo cha habari kwa maslahi yake binafsi.
 
Walisema kuwa wanampongeza raisi kwa kauli yake mbiu ya “HAPA KAZI TU” kwa kuwa inawapa motisha wananchi wa kufanya kazi kwa bidii. Lakini walishangazwa na raisi huyo baada ya kutoa onyo kwa Bw. Makonda kwa alichokifanya lakini matokeo yake ameweza kupongeza kwa kumwambia wewe piga kazi tu usisikilize maneno yao hii inaonyesha kuwa raisi John Pombe Magufuli karidhika na kitendo iko.
Waandishi wa habari wakiwa kazini