Zinazobamba

RAHCO YAPIGILIA MSUMARI UBOMOAJI KWA WAVAMIZI WA HIFADHI YA RELI,SOMA HAPO KUJUA


Mkurugenzi mtendaji  Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi  habari leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia  zoezi la ubomoji wa nyumba zilizopo kwenye hifadhi ya reli


 Afisa Uhusiano wa RAHCO,Catherine Moshi  akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam

NA KAROLI VINSENT
 Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyomo katika hifadhi ya reli linaloendelea nchini limezingatia taratibu na sheria za uendeshaji wa reli na kwamba matangazo ya notisi ya kuwataarifu waanchi waliovamiwa hifadhi hizo zilizotolewa mapema ili wananchi hao waweze kuhama.

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji RAHCO Bw. Massanja Kadagosi amesema Ubomoaji huo unaoendelea haupo kwa ajili ya kumuonea mtu bali upo kwa ajili ya kulinda miundombinu ya reli ikiwemo pia kujali usalama wa wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli.

‘’Sheria ya Reli Na.4 ya mwaka 2002,kifungu cha 57 (2) kinabainisha kuwa mtu yoyote haruhusiwi kufanya ujenzi wowote katika hifadhi ya njia ya reli pasipo kibali cha RAHCO, kwani sheria hii inatamka wazi  kuwa mtu yeyote harusiwi kufanya ujenzi wowote katika eneo lilopangwa na mamlaka husika”

Madagosi amesema kabla ya kuanza kuzibomoa nyumba hizo walitoa notisi mbali mbali ikiwemo tangazo la kuwataarifu wavamizi hao kupitia kwenye vyombo vya habari vya tarehe 25/4/2016, pamoja na kutoa barua kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ya kuwajulisha wananchi hao kuanza kuhama kabla yauvunjaji kuanza.


Mbali na Barua hizo, amesema Bw. Kadagosi  tarehe 9 hadi tarehe 10 /2/2017 waliziweka nyumba alama ya X kwa wavamizi hao, analosema kuwa watu wanaosema wananchi hao wanaovunjiwa hakuwapata taarifa za kutakiwa kuvunjiwa nyumba si za kweli kwani taarifa zilitolewa.