Zinazobamba

LICHA YA MAGUFULI "KUMKINGIA KIFUA' RC MAKONDA ALIKOROGA VIBAYA,JENERALI ULIMWENGU,ZITTO KABWE,MBWANA SAMATA WATEMA CHECHE,SOMA HAPO KUJUA

 Mwandishi wa habari Nguli nchini,,Jenerali Ulimwengu naye afunguka sakata la Makonda kuvamia kituo cha Clauds
Akihijowa na DW mchana huu Jenerali Ulimwengu ameshauri Makonda ashitakiwe...

Amesema ni tukio linaloweza kufanywa na viongozi ambao wanajiona hawana mipaka katika utawala wao.

Amesema mkuu wa mkoa amelewa madaraka na kwa kufanya tukio hilo ameonyesha kwamba hana kitu chochote kinachoweza kumzuia. Amewaomba wananchi kupata sauti zao katika kutetea haki zao.

Amesema suala la Makonda kuwajibishwa linategemea na mtu aliyemchagua ambaye ndiye kiongozi wa nchi kwa hiyo Raisi akiona kwamba kuna haja ya Makonda kuwajibishwa basi amuwajibishe ili iwe fundisho na kwa viongozi wengine 
 
Zitto Kabwe afunguka,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe naye hakuwa nyuma kulizungumzia sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda la kuvamia kituo cha Tv cha Clauds Media,baada ya kuwataka wanahabari kususia kuandika habari za serikali,soma hapo kujua
Mchezaji wa Kitanzania anayekipiga soko nchi za Ulaya,Mbwana Samata amefunguka haya,,,,,,
 
BAADA ya kuvamiwa kwa Kituo cha Redio cha Clouds Fm, imeibuka mijadala mingi, Watanzania wakaijadili kila kona ya nchi. Katika mijadala hiyo, wapo wanasiasa, watumishi wa umma, waumini wa dini na wanamichezo ambapo mchezaji wa Taifa Stars anayekipiga nchini Ubelgiji katika Klabu ya Genk, Mbwana Samatta amefunguka kuwa wanasiasa wanakosa maadili.

“Ndiyo maana siasa imekuwa cheap maana viongozi wenyewe wana-hang out na akina Amber Lulu na Gigy Money” aliandika Samatta.