Zinazobamba

KITABU CHA UWIANO WA TAKWIMU ZA WANAWAKE NA WANAUME CHAZINDULIWA JIJIJINI DAR ES SALAAM

 Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku (katikati) akiwa na wadau wakionesha kitabu cha uwiano wa takwimu za  wanawake na wanaume wakati wa hafla ya kuzindua kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango, Ofisa wa Takwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger, Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda na Mwanahabari Philip..Kitabu hicho kimeandikwa na wanafunzi watano kutoka Tanzania waliopata mafunzo ya miezi 11 nchini Sweden.
 Mada kuhusu mafunzo hayo zikitolewa kabla ya uzinduzi.

 Wafadhili wa mafunzo hayo kutoka nchini Sweden wakifuatilia mada kuhusu mafunzo hayo.
 Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango (kushoto) na Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa karibu hafla hiyo.
 Mtakwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda akichangia jambo
 Mada zikiendelea kutolewa.
 Mhadhiri kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki (kushoto), akizungumzia mafunzo ya takwimu waliopata nchini Sweden.
 Mratibu wa masuala ya Jinsia wa Tacaids, Jacob Kayombo akichangia jambo katika mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Jerome Kamwela akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina akichangia.
 Washiriki wa  mafunzo hayo (walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa. Kutoka kulia  Ofisa kutoka HakiElimu, Joyce Mkina, Mhadhiri kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashairiki, Chisker Masaki, Ofisa wa Jinsia wa Tacaids, Judith Luande, Philbert Mrema kutoka NBS na Mariam Kitembe kutoka NBS.

Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale

WANAUME wameonekana kuwa wengi katika nafasi mbalimbali ukilinganisha na wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo cha Takwimu Afrika Mashariki, Chisker Masaki wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Uwiano wa Taarifa za Takwimu kwa Wanawake na Wanaume Tanzania.

Alisema kitabu hicho kimeandaliwa na washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa za takwimu kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Hakielimu , Ofisi yaTaifa ya Takwimu (NBS) na Chuo cha Takwimu cha AfrikaMashariki, chini ya wakufunzi  wa masuala ya ukusanyaji wa taarifa kutoka nchini Sweden.  

Masaki alisema utafiti unaonesha  kuwa kuna tofauti  kubwa   za  uwiano kati ya  mwanamke na mwaume katika  nyanja za kimaendeleo na kijamii, ambapo maeneo mengi  yanaonekana kutwaliwa na wanaume kuliko wanawake.

Akitolea  mfano  upande  wa  elimu  kuanzia  shule  za  msingi  hadi  chuo  kikuu  wasichana  wanaoandikishwa  hadi  kufikia  chuo  kikuu  ni  wachache  ukilinganisha  na  wavulana,watu  wenye  nafasi  nzuri maofisini  hasa  ngazi  za  Ukurugenzi  na  mameneja  wengi ni wanaume  ukilinganisha na   wanawake,viongozi  wa  kisiasa mfano  mawaziri na wabunge wanawake ni wachache ukilinganisha na wanaume.

Alisema pamoja na uwiano huo wa wanaume kuwa kiwango kikubwa katika  masuala ya maendeleo wanawake wamekuwa wakichukua  nafasi kubwa katika kuathirika na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Mafunzo  hayo ya ukusanyaji wa taarifa yalianza tangu mwaka 2016 mwezi Mei hadi Machi  2017  ambapo mafunzo yalifanyika nchini Sweden ni ukusanyaji wa taarifa pamoja na uandaaji wake kitabu ukafanyika Tanzania.