MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AIANGUKIA CHADEMA KUHUSU UKUTA,NAO JUMUIYA YA KIKRISTO KUTOA TAMKO KALI,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
MSAJILI wa vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi
amekiangukia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na Chama
cha Mapinduzi (CCM) ambavyo vyama hivyo
vilivyopanga kuandamana kwa nyakati tofauti ,kusitisha maandamano hayo.
Amesema wasitishe maandano hayo ili kupisha mazungumzo
ambayo yatafanyika kwenye Baraza la
vyama vya siasa ambalo linatarajia kukutana tarehe 29 na tarehe 30 ya mwezi huu.
Jaji Mtungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam
wakati wa mkutano na waandishi wa habari huku akivitaka vyama hivyo kuacha kufanya maandamano hayo ili
suluhu ipatikanekatika baraza hilo.
Amesema Baraza hizo linaloundwa na vyama 20
vilivyopewa usajili litakuwa na lengo la kujadili mambo mbali mbali yanayohusu
vyama hivyo.
Kuibuka kwa kauli hii ya msajili wa vyama Siasa
nchini inakuja siku moja kupita baada ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha)
kutangaza kuwa maandamano hayo kuwa yako pale,licha ya kutolewa katazo kutoka jeshi
la polisi.
Mbali na Bavicha pia Umoja wa Vijana wa chama cha
Mapinduzi UVCCM pia nao wametangaza kufanya maandamano kuanzia 31 Agoust mwaka
huu kwa kile wanachodai kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua anazofanya.
JUMUIYA YA
WAKRISTO WAJIPANGA KUTOA NENO.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa Fullhabari.blog
aliyoko ndani ya jumuiya ya Kikristo
nchini (CCT) ambaye hakutaka kutotajwa jina lake mtandaoni,amesema CCT
wanasikitika na hali ya kisiasa
inayotokea nchini huku wakitahadhalisha kuwa nchi kuingia kwenye msuguano.
“Yaani kwa sasa hali inapoelekea nchini ni mbaya
sana,yaani kama hawa viongozi wasipoweka tofauti pembeni,basi Taifa litaingia
kwenye uhasama ambao unaweza ukarudisha nyuma maendeleo,kwahiyo sisi viongozi
wa dini lazima tuibuke na kutoa tamko,kulaani”amesema Mtoa taarifa huyo ambaye
pia ni mchungaji wa kanisa moja hapa nchini.
Amesema hatua ya maandamano na mikutano ya hadhara
ambayo wanasiasa wanaitaka huku Polisi wakikitaza ,amedai njia hiyo haitaweza
kumaliza msuguano huu.
“Sisi viongozi wakiroho hatuwezi tukaa kimya huku
Amani ya nchi inaweza ikapoteka kutokana na misuguano hii,lazime tukemee na
kuwataka viongozi wamalize misuguano,hata hiyo serikali ya viwanda hawezi
kutimia kwa misuguano hii,hapa lazima suluhu ipatikane”ameongeza Kiongozi huyo
wa kiroho.