DPP AANZA KUONG'OLEWA MENO,MAHAKAMA KUU YAMZUIA TABIA YAKE YA KUZUIA RUFAA,SOMA HAPO KUJUA
MAMLAKA ya kugomea dhamana za watuhumiwa aliyokuwa
nayo Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), sasa imeondolewa na
mahakama kuu.
Awali, DPP alikuwa na uwezo wa kuzuia dhamana
za baadhi ya watuhumiwa kwa namna alivyoona inafaa licha ya kuwepo kwa
malalamiko ya uhalali wa kuzia dhamana hizo.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikitolewa na
DPP ni maslahi ya umma hivyo kusababisha haki ya kupata dhamana kuwa
ngumu.
Kwa kuwa hatua hiyo inakiuka Katiba ya Tanzania,
Mahakama Kuu imefikia uamuzi wa kumwondolea mamlaka hayo DPP.
Kifungu kilichokuwa kikimpa mamlaka DPP ya kuzuia
dhamana ni 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na kwamba,
kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya Tanzania.
Uchambuzi wa udhaifu wa kifungo hicho kilichokuwa
kikitumiwa na DPP ulitolewa na Majaji Sekieti Kihiyo na Dk. John Ruhangisa
wakiongozwa na Jaji Kiongozi Shaaban Lila.
“Imeamriwa mtuhumiwa aliye chini ya
ulinzi wa polisi au mtuhumiwa yoyote, anatakiwa kupewa haki yake ya kujitetea
kabla ya haki hiyo haijazuiliwa na mkurugenzi wa mashitaka kwa pingamizi la
kuwanyima dhamana,” sehemu ya taarifa ya majaji hao
imeeleza hivyo.
Kifungu cha 148 (4) kinasema; “bila kujali
kitu chochote kilichopo kwenye kifungu hiki, hakuna afisa polisi wala mahakama
atakayeweza, baada ya mtu kukamatwa na wakati anasubiri shauri au rufaa,
atathibitisha kwa maandishi kwamba kuna uwezekano kwa usalama au maslahi ya
Jamhuri.
“…na cheti kilichotolewa na Mkurugenzi
wa Mashitaka chini ya kifungu hiki kitaanza kutumika kuanzia terehe
kitakapowasilishwa mahakamani au kutaarifiwa kwa afisa msimamizi wa kituo cha
polisi na kitaendelea kutumika hadi mwenendo utakapohitimishwa ama mkurugenzi
wa mashitaka atakapokiondoa.”
Kuondolewa kwa mamlaka ya DPP kuzuia dhamana za
watuhumiwa kulitokana na kupelekwa pingamizi la kikatiba lililowasilishwa na
Jeremiah Mtosebya, Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye amesema kifungu hicho
kinakiuka Katiba ya Tanzania.