BAADA YA TUNDU LISSU DHAHAMA LA KESI LAHAMIA KWA MBUNGE KUBENEA,NI MWENDELEZO KWA WABUNGE WA UPINZANI,SOMA HAPO KUJUA
SAED Kubenea Mbunge wa Jimbo la Ubungo
amejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuhojiwa
kabla ya kupewa dhamana kufuatia tuhuma za kuandika makala inayodaiwa kuwa ya
uchochezi kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar, anaandika Faki Sosi.
Kubenea ambaye pia Mkurugenzi
wa Hali Halisi Publishers inayomiliki magazeti ya MwanaHALISI na MSETO anadaiwa
kufanya uchochezi kwa kuandika makala katika gazeti la MwanaHALISI toleo la 349
la Julai 25-31 yenye kichwa cha habari, ‘Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?’
Kubenea amefika katika kituo hicho cha Polisi leo
saa saba na robo mchana (13:15) akiwa na Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Frederick Kihwelu wakili
mwandamizi wa Chama hicho.
Baaada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa mawili, saa
tisa na robo alasiri (15:45) alitoka na kuondoka huku wandishi wa habari
wakishindwa kuzungumza naye baada Jeshi la Polisi kuwazuia waandishi wa habari
kuingia katika eneo la kituo hicho.
Akizungumza kwa njia ya simu, Lissu ambaye ndiye
mwanasheria wa Kubenea katika sakata hilo amesema kuwa, Kubenea amehojiwa kwa
madai ya uchochezi lakini alichokiandika ni hali halisi ya Zanzibar hususani
visiwa vya Pemba.
“Kubenea amechiwa kwa dhamana na ameamriwa kurudi
tena kituoni hapo tarehe 18 Agosti, mwaka huu,” amesema Lissu.
Katika makala yake inayodaiwa kuwa ni ya kichochezi
iliyokuwa na kichwa cha habari, “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?” Kubenea
alielezea jinsi Jeshi Polisi Visiwani Pemba wanadaiwa kuwabambikia kesi
wananchi, kuwapiga na kuwatesa kwa madai kuwa wananchi hao wanaipinga serikali.
Kubenea aliandika Makala hiyo baada ya kusafiri
kutoka Dar es Salaam Mpaka Zanzibar kufuatilia kile alichokitaja kama mateso,
unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi wasio na hatia
visiwani humo.
Miongoni mwa vijana na wahanga wa kubambikiwa kesi,
kupingwa na kuteswa visiwani Pemba waliotajwa na Kubenea katika makala yake ni
ni Hijja Hassani aliyetangazwa kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani kabla ya
Jecha Salim Jecha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta
uchaguzi.