NI MAPAMBANO YAMEANZA DODOMA NI KATI YA POLISI,BAVICHA NA CCM YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
KATIKA harakati za kuhakikisha wafuasi
wa vyama vya upinzani nchini zinazimwa, Jeshi la Polisi mkoani Dodoama
limewatia mbaroni viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),anaandika Dany Tibason.
Waliokamatwa na jeshi hilo ni viongozi wa kitaifa wa Baraza la
Vijana la Chadema (Bavicha) wakiwa wanakula na kunywa katika
Bar ya Cape Town mjini humo.
Hata hivyo zoezi
la kuwakamata viongozi hao linaendelea hata pale ambapo mtu yoyote anayeonekana
kuwa, amevaa fulana zenye maneno yenye kaulimbiu za Chadema.
Tukio hilo
limekuja ikiwa ni siku chache tangu jeshi hilo, kuzuia mahafali ya Umoja wa
Wanavyuo Chadema (CHASO) kwa kuamuru wahusika waliokuwa wamekusanyika kwenye
Hoteli ya African Dreems, mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick
Sumaye kutawanyika.
Askari wenye
mabomu ya machozi, silaha za moto na gari moja la maji ya kuwasha, walizunguka
eneo la hoteli hiyo huku kiongozi wa polisi akitangaza;
“Ilani, ilani,
imeamriwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, wote mliokusanyika mahali hapo
mtawanyike, vinginevyo nguvu itatumika.”
Mahafali hayo
hayakufanyika kwa wanavyuo na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani,
kuondoka eneo hilo huku serikali mkoani humo ikieleza kuwa chanzo ni taarifa za
uwepo wa ugonjwa wa ajabu, uliyodaiwa kuibuka wilayani Chemba na Kondoa.
Hata hivyo, siku
chache baadaye, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alitangaza zuio la
kufanyika mikutano ya kisiasa ya hadhara na ya ndani pamoja na maandamano
akisema wakati wa uchaguzi umepita shughuli za kisiasa zipumzishwe mpaka
kipindi cha uchaguzi ujao, ili watu wafanye kazi za maendeleo.
Akizingumza kwa
njia ya simu leo Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,
amethibitisha viongozi wa Bavicha kukamatwa wakituhumiwa kukusudia kuhamasisha
kuikashifu serikali.
Amesema,
hawatadhaminiwa mpaka Jumatatu, watakapofikishwa mahakamani.
Joseph
Kasambala, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema-Taifa ametaja waliokamatwa kuwa ni
Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha- Taifa, Julius Mwita, Katibu wa Bavicha
-Taifa na George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Mbeya.
Akielezea
ilivyotokea, Kasambala amesema, walikuwa katika ziara kwenye baadhi ya mikoa,
walianzia mkoani Mara, katika Kijiji cha Mwitongo, Mwanza kabla hawajafika
Dodoma juzi Saa 8:00 mchana.
Amesema leo
walikusudia kukutana na vyombo vya habari mjini Dodoma, kuelezea hatua
iliyofikiwa katika mpango wao wa Bavicha – Taifa kushirikiana na Jeshi la
Polisi mkoani Dodoma, kuzuia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya
mkutano mkuu wa taifa, 23 mwezi huu.
Amesema, wakiwa
Cape Town, majira ya usiku aliwaacha wenzake na kwenda kukutana na jamaa yake
mwingine na kwamba baadaye alipata taarifa za wenzake kukamatwa na polisi.
Amesema
kilichomsikitisha ni kukataliwa kuonana nao, alipofika kwenye kituo cha polisi
cha kati jana asubuhi ambapo alitakiwa kwanza akaonane na viongozi wa polisi wa
wilaya na mkoa (OCD, RPC).
Pia ameeleza
kwamba, taarifa alizopatiwa kwenye kituo hicho cha polisi zimeeleza kuwa kosa
wanalotuhumiwa kufanya ni kuikashifu serikali, kwa kuvaa T/shirt yenye
maandishi “Dikteta Uchwara”.
Hata hivyo,
Kasambara amesema, madai hayo ni ya uongo huku akionesha maandiko yaliyo kwenye
fulana aliyokuwa amevaa, yenye rangi nyeusi na maandiko meupe yanayosema;
“Mwl. Nyerere;
Demokrasia inanyongwa” upande wa mbele huku upande wa nyuma ikisomeka; “Haki na
Amani.
Amesema, ziara
yao inajumuisha viongozi sita wa Bavicha, akiwataja kuwa pamoja na yeye, watatu
waliokamatwa ni Edward Simbeye, Katibu Mwenezi wa Bavicha–Taifa na Katibu wa
Bavicha – mkoani Temeke, Hilda.