Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Awazuia Vijana wa Chadema ( BAVICHA ) Kwenda Dodoma Kuzuia Mkutano wa CCM
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza kusitisha
mpango wa vijana wa chama hicho kwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM
ili kuepusha maafa ambayo yanaweza kutokea. Badala yake, Mbowe amesema
wataendelea kusaka haki ya kufanya mikutano ndani na nje ya nchi.
Sambamba na uamuzi huo, chama hicho kimetaka viongozi sita wa Baraza la
Vijana (Bavicha) wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuachiwa mara moja.
Mbowe alitoa tamko hilo jana wakati akizungumza na wanahabari jijini
Arusha, katika mkutano wa mameya na wenyeviti wa halmashauri 18
zinazoongozwa na Umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa).
Sababu za
kusitisha
Mbowe alisema wamewataka vijana wa Chadema nchi nzima ambao walianza kujiandaa kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia mkutano huo wa Julai 23 kutokwenda kwa sababu polisi wamepewa maagizo ya kuwapiga na kuwajeruhi, hivyo wao hawataki kupambana nao.
Mbowe alisema wamewataka vijana wa Chadema nchi nzima ambao walianza kujiandaa kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia mkutano huo wa Julai 23 kutokwenda kwa sababu polisi wamepewa maagizo ya kuwapiga na kuwajeruhi, hivyo wao hawataki kupambana nao.
“Nawataka vijana wote wa
Chadema waliokuwa wanajiandaa kwenda Dodoma wasitishe na wasubiri
maelekezo mapya ya Chadema,” alisema Mbowe.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema wana taarifa Jeshi la Polisi
limejipanga kuwanyima dhamana viongozi wa Bavicha hadi baada ya mkutano
wa CCM, ingawa viongozi wote wa chama hicho hawana hofu ya kukaa
mahabusu.
Aliwataka vijana hao kutokwenda Dodoma na wawaache CCM
waendelee na mkutano wao kwa kuwa Chadema haina hofu na mkutano wa chama
hicho, bali walitaka dunia ione jinsi polisi wanavyofanya kazi kwa
maelezo ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi.
“Wakati sisi tunazuiwa kufanya siasa, Rais anafanya siasa, Waziri Mkuu
anafanya siasa, mawaziri wanafanya siasa, wakuu wa mikoa na wilaya
wanafanya siasa jambo ambalo si sahihi,” alisema.
Alisema lengo la
Bavicha kwenda Dodoma ni kuchoshwa na uonevu wa kuzuiwa kufanya mikutano
ya ndani na hadhara wakati CCM wanaendelea na mikutano yao.
“Waliona
pengine itakuwa busara washinikize polisi kuona maagizo yao ya kuzuiwa
mikutano yanatekelezwa kwa wote,” alisema.
Alilitaka jeshi la polisi
kufanya kazi kwa kufuata taratibu kwa kutoa haki sawa kwa wote, kwa
kuruhusu vyama vyote kufanya mikutano yao.
Apinga tamko la Mwigulu
Kuhusu tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu mikutano hiyo, Mbowe alisema hawakulielewa tamko hilo la Rais, kuwa mikutano ambayo imezuiwa ni ya hadhara na maandamano na si ya ndani.
Kuhusu tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu mikutano hiyo, Mbowe alisema hawakulielewa tamko hilo la Rais, kuwa mikutano ambayo imezuiwa ni ya hadhara na maandamano na si ya ndani.
Alisema mikutano ya ndani ya chama hicho imezuiwa kwani Chadema Wilaya
ya Kahama walikuwa na mkutano wa ndani wa uchaguzi ambao umezuiwa.
Alisema mkutano wa ndani na wabunge wa Chadema mkoani Shinyanga ulizuiwa
na pia mahafali za Vijana wa Vyuo Vikuu wa Chadema (Chaso).
“Lakini
wakati haya yanafanyika, CCM waliendelea na mikutano yao na mahafali
yao,” alisema.
Alisema Chadema itaendelea kudai haki ya mikutano na
maandamano katika mahakama za ndani na nje ikiwamo ya Afrika ya
Mashariki.
Viongozi wa madiwani
Katika mkutano wa wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Chadema, Mbowe alisema Calist Lazaro, Meya wa jiji la Arusha amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa madiwani wa Chadema nchini.
Katika mkutano wa wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Chadema, Mbowe alisema Calist Lazaro, Meya wa jiji la Arusha amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa madiwani wa Chadema nchini.
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob
alichaguliwa kuwa katibu wa madiwani wote wa chama hicho na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Tarime, Moses Matiku alichaguliwa kuwa mnadhimu wao.
Wote hao watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu Chadema.
Katibu Mkuu wa Chadema,
Dk Vincent Mashinji alisema katika mkutano huo wenyeviti hao wamepatiwa
elimu juu kuongoza vyema halmashauri zao ili kuchochea maendeleo.
“Siku
mbili za mkutano huu tumekaa na kuweka mikakati bora ya kuhakikisha
halmashauri zinazoongozwa na upinzani zinafanya vizuri,” alisema.