WAKUU WA VYUO VYA USTAWI WA JAMII WAELEZWA SIRI YA KUZALISHA WATAALAM WENYE SIFA.
Serikali imewataka Wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini
kufanya kazi kwa kuzingatia weledi , kanuni, miongozo na taratibu
zinazosimamia uendeshaji wa vyuo hivyo ili kuiwezesha sekta hiyo kupiga
hatua kwa kuzalisha wataalam wenye sifa wanaokidhi matarajio ya
wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma
na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Erasimus Rugarabamu
wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Sihaba Nkinga.
Bw.
Rugarabamu amewataka wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuendelea
kusimamia kwa umakini mkubwa wa Rasilimali za vyuo hivyo na kubainisha
kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mkuu
wa Chuo yeyote atakayeshindwa kuzingatia weledi , kanuni na taratibu
zinazosimamia uendeshaji wa vyuo hivyo.
" Ninyi
ndio wasimamizi wa uzalishaji wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini,
mnao wajibu wa kubadilisha fikra za wananchi na kuwa chachu ya
maendeleo, hakikisheni mnasimamia vizuri suala la udahili wa wanafunzi
kwa kuwa na wanafunzi wenye sifa.
Aidha,
amewataka wakuu hao wa vyuo kuhakikisha kuwa wanapiga vita kwa vitendo
udahili wa vyeti vya kughushi ( vyeti feki) akisisitiza kuwa Serikali
haitasita kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa Mkuu wa Chuo
yeyoye atakayehusika kwa namna moja au nyingine kusaidia udahili wa
wananfunzi wasio na sifa.
Ametoa wito kwa wakuu
na Wakuu wa taaluma wa vyuo hivyo kuwa makini katika suala la udahili
wa wanafunzi wanaojiunga katika fani ya maendeleo ya jamii ili kuendelea
kujenga heshima ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii na kutimiza matarajio
ya kuwaletea maendeleo wananchi.
" Hakikisheni
mnaepuka maslahi binafsi katika usimamizi wa taaluma, suala la vyeti
feki lisiwe na nafasi katika vyuo vyetu, fanyeni kazi kwa kuzingatia
sheria ili tuendelee kutoa wahitimu bora" Amesisitiza Rugarabamu.
Katika
hatua nyingine amewataka wakuu hao kuwa wabunifu ili vyuo
wanavyovisimamia viweze kuhimili soko la ushindani kutoka vyuo vingine
vya elimu ya Maendeleo ya jamiii hapa nchini ili vyuo chini ya wizara,
viweze kutekeleza majukumu kwa ufanisi na kuzalisha wataalam wanaokidhi
mahitaji ya soko.
" Ili vyuo vyetu viendelee
kuonekana lazima viweze kuhimili ushindani kutoka katika vyuo vingine
vinavyotoa taaluma kama hii, jambo hili lazima tulifanye kwa nguvu ili
tuendelee kuwa wazalishaji bora wa wataalam wa elimu ya Maendeleo ya
Jamii hapa nchini" Amesisitiza Rugarabamu.
Aidha, ametoa wito kwa wakuu hao kusimamia vizuri rasilimali za fedha
Upimaji
wa Wazi (OPRAS) Amesema kuwa watumishi wote wa Serikali lazima wapimwe
utendaji kazi wao kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na kusisitiza kuwa
jambo hilo ni lazima
Aidha, amewataka Wakuu
hao kuhakikisha kuwa wanavisimamia vyuo wanavyoviongoza kwa mujibu wa
sheria na kuhakikisha kuwa wanawasilisha taarifa kuhusu maendeleo ya
vyuo vyao kwa lengo la kuiwezesha Serikali kuchukua hatua za katika
maeneo ambayo hayaendi vizuri kuviwezesha vyuo hivyo kupiga hatua
kitaaluma.
Awali akizungumza kabla ya ufunguzi
wa mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara hiyo
Bw. Enterberth Nyoni amesema kuwa Mkutano huo ni muhimu sana kwa kuwa
umewakutanisha wakuu wa Vyuo na Makamu Wakuu wa Vyuo wanaozalisha
Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini ambao huajiliwa na Serikali katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa, taasisi na Mashirika mbalimbali.
Amesema
kuwa kufanyika kwa mkutano huo kuna umuhimu mkubwa katika maendeleo ya
nchi kupitia mchango wa maafisa maendeleo ya jamii ambao husimamia
shughuli za maendeleo ya wananchi kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi
Taifa pia usimamizi na utoaji wa elimu kuhusu Haki za makundi mbalimbali
katika jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Paschal Joseph Mahinyila
amesema kuwa vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinaendelea kufanya kazi nzuri
ya kuzalisha wataalam wa masuala ya maendeleo ambao wamekua msaada kwa
wananchi.
Amesema kuwa Serikali inaendelea
kuifanyia kazi changamoto ya uhaba na uchakavu wa majengo inayovikabili
baadhi ya vyuo vya maendeleo ya Jamii ili viweze kudahili wanafunzi
wengi zaidi na kuendelea kutoa elimu katika mazingira bora.
Aidha,
amesema kuwa kupitia kikao kazi hicho changamoto ya Miongozo ya
uendeshaji itaweza kufanyiwa kazi ili vyuo vyote viweze kuzungumza lugha
moja na kutekeleza matakwa ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE) pamoja na kuviwezesha vyuo vingine vya maendeleo ya jamii
vilivyo chini ya wizara hiyo kuanza kutoa wahitimu wa shahada ya kwanza
kwa kujiunga na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Arusha.
Naye
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rugemba, Mafinga mkoani Iringa Bi.
Santina Mbata akizungumzia mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho
amesema kuwa kukutana kwa wakuu hao wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni
fursa pekee inayowapa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kisera,
kisheria, taratibu na miongozo mbalimbali inayosimamia vyuo hivyo.
Bi.Santina
ameeleza kuwa licha ya chuo anachokiongoza kukabiliwa na changamoto
mbalimbali Serikali inaendelea kukijengea uwezo ili kuhakikisha kuwa
kinaendelea kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuendelea
kuwajengea uwezo wananchi wanaopata mafunzo kukabilina na changamoto
mbalimbali za maendeleo ya wananchi.