RAIS MAGUFULI APUUZWA MCHANA KWEUPE,NA DC NA MKUREGENZI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
MARRY Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mwanza na
Housian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la hilo wamekiuka agizo la Rais John
Magufuli la kufanyika kwa sherehe za kupongezana pindi mtumishi wa umma
anapoteuliwa kushika nyadhifa, anaandika Moses Mseti.
Machi mwaka huu, Rais Magufuli
akiwaapisha wakuu wa mikoa jijini Dar e Salaam, aliwataka kutosherehekea
kuteuliwa kwao na kwamba, wafanye hivyo siku wakitimuliwa.
Rais
Magufuli pia aliwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwekeza nguvu zao katika kuondoa
tatizo sugu la madawati kwenye shule za umma, agizo ambalo muda wake
ulikamilika Juni 30 mwaka huu huku Mkoa wa Mwanza ukikwama kufikia malengo
hayo.
Sherehe
za kumkaribisha mkuu huyo wa Wilaya ya Nyamagana na kumuaga aliyekuwa Mkuu wa
Wilaya hiyo, Baraka Konisaga maarufu mtumishi wa Mungu, ziliandaliwa na
Halmashauri ya Jiji la Mwanza chini ya kaimu mkurugenzi huyo.
Sherehe
hizo zilizofanyika katika Hoteli ya New Mwanza ambapo zaidi ya watu 100
wakiwemo watumishi wa Jiji la Mwanza wakihudhuria ambapo kiasi cha zaidi ya Sh.
30 milioni zikitajwa kutumika.
Sherehe
hizo zilizoanza saa 12 jioni hadi saa 4 usiku, waandishi wa vyombo
mbalimbali vya habari walitimliwa na kutakiwa kutoripoti habari hii.
Awali,
waandishi walialikwa na baadhi ya viongozi hao wakiwemo wakuu wa
wilaya kwa ajili ya kuripoti lakini baadaye ikaibuliwa hoja ya kwamba, inaweza
kusababisha tatizo hasa kutokana na kutokamilika kwa fedha za ununuzi wa
madawati.
Hosian
Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo alipotafutwa kuzungumzia suala hilo
amesema kuwa, fedha zilizotumika kuandaa sherehe hiyo hazikutoka katika mfuko
wa serikali na kwamba, walichangishana baadhi ya watumishi wa jiji na taasisi
mbalimbali.
“Wewe
kama ulivyoona mwenye katika sherehe hiyo yalikuwepo makundi mbalimbali,
ikiwemo Mwauwasa (Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira) mkoani Mwanza na
sio fedha kutoka Jiji,” amesema Kusiga ambaye pia ni Ofisa Mipango wa Jiji.
Tesha,
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akizungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha
zilizotumika katika sherehe hiyo sio fedha za serikali.
“Pesa
zilizotumika sio za serikali, unaniuliza fedha zilizochangwa eti kwanini
hazijapelekwa kwenye madawati, mimi ningewakataza wasifanye sherehe, hivi wewe
vipii… mbona sikuelewi,” amesema.