Zinazobamba

BAVICHA WAIENYESHA POLISI NA DDP WAO MAHAKAMANI,WAJIUMAUMA KUHUSU HATI YA MASHTAKA,SOMA HAPO KUJUA



Katibu Mkuu wa BAVICHA, Julius Mwita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya vijana kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ngazi ya jimbo na kata.


JESHI la Polisi mkoani  Dodoma limejikuta katika wakati mgumu kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani viongozi wa wakuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), anaandika Dany Tibason.

Jeshi hilo limeshindwa kuwapandisha kizimbani viongozi hao na kutuwatupia mpira mwendesha mashitaka wa serikali(DPP), kwa madai kwamba alikosekana katika kuandaa hati ya mashitaka na kulazimika kuiandika upya jambo lililosababisha kuchelewa kwa muda wa kuwapeleka watuhumiwa mahakamani.

Mbali na jeshi hilo kushindwa kuwafikisha watuhumiwa katika mahakama pia jeshi la polisi limeendelea kupigilia msumali kwa kuwanyima dhamana watuhumiwa hao kwa madai kwamba kesi yao ambayo inawakabili viongozi hao haina dhamana hadi watakapokuwa wamefikishwa mahakamani.


Kauli hiyo imetolewa leo na Lazaro Mambosasa, Kamanda wa jeshi hilo Mkoa wa Dodoma, alipokuwa akijibu maswali ya mwandishi wa habari hizi kwa kutaka kueleza ni kwanini watuhumiwa hao hawakuweza kufikishwa mahakamani kama alivyokuwa amehaidi wakati apozungumza na waandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao wangefikishwa mahakamani siku ya jumatatu.

“Wao watuhumiwa hawatafikishwa leo watafikishwa kesho,na kilichosababisha kutofikishwa mahakanani ni kutokana na mambo ya kisheria kidogo ambayo yanatokana na mwandaaji wa mashitaka ambaye ni mwanasheia wa serikali.
“Sisi kila kitu tulishamaliza na mahojiano tulishamaliza lakini mwandaji wa mashitaka aliandaa hati ya mashitaka(chaji) lakini alikosea na kulazimika kuirudia  na ndipo muda ukawa umepita na ndiyo sababu ya kutoweza kuwafikisha mahakamani.

“Kuhusiana na suala la dhamana kesi hiyo haina dhamana tusubiri huko huko mahamani” alisema Mambosasa.

Kuhusiana na tukio la watumuhiwa hao kutenganishwa katika mahabusu alisema kuwa hilo ni jambo la kawahida kwa watu wenye kesi inayofanana kutenganishwa na jambo hilo halina tatizo yotote.

“Ni jambo la kawaida sana kwa watu waliokamatwa kwa kosa moja ili uweze kufanya mahojiano ni lazima uwatenganishe na jambo hilo siyo kwao tu ni jambo la kawaida kwa watu wote” alisema Mambosasa.

MwanaHALISI Online imebaini kuwa viongozi hao wakiwa rumande jeshi la polisi liliwafanyia upekuzi katika vyumba vyao walipofikia Katika nyumba ya kulala wageni ya Drive Inn iliyopo Dodoma Mjini, waliwatenganisha watuhumiwa hao kwa kuwapeleka katika selo ya Chamwino Ikulu iliyopo wilayani Chamwino.

Waliopelekwa katika selo ya Chamwino ni pamoja na Patrobas Katambi Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Joseph Kasambala Mjumbe wa Baraza Kuu Bavicha, na George Tito Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Mbeya, ambapo Juliasi Mwita Katibu wa Bavicha taifa akiwa ameachwa katika kituo cha polisi cha kati.
Viongozi hao ambao walikamatwa tangu siku ya Ijumaa kuamkia jumamosi wiki iliyopita hadi jana jumatatu wameendelea kusota rumande kwa kukosa dhama.

Viongozi hao walikamatwa wakiwa katika wakiwa katika bar ya Cape Town wakiwa wanapata chakula na vinywaji huku wakiwa wamevalia t-shert ambazo lilikuwa na ujumbe ambao ulikuwa ukisomeka Mwl .Nyerere Demokrasia Inakanyagwa huku mbele kukiwa kuna maandishi ambayo yalikuwa yameandikwa ‘amani = haki’

Kwa upande wake Patrick Ole Sosope Kaimu wa Mwenyekiti wa Bavichaa Taifa, amesema amesikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kushindwa kuwafikisha mahakamani viongozi hao huku wakirushiana mpira kati ya jeshi hilo na mwanasheria wa serikali.

“Inasikitisha kuona jeshi la polisi likishindwa kuwafikisha viongozi hao kwa wakati licha ya kuwa waliwakamata toja ijumaa huku wakiwa hawana makosa
.
“Sisi tunaamini kuwa viongozi hao hawana makosa yoyote na kama wana makosa ni kwanini wasiweze kufikishwa mahakamani na tangu asubuhi tuko hapa.

“Viongozi hao walikamatwa tangu Ijumaa na sasa leo ni juma tatu kana ni taratibu za kisheria wanatakiwa kufikishwa mahakamani kwa muda usiozidi saa 24 lakini cha kusikitisha sana tangu asubuhi.

Viongozi hao walitakiwa kuletwa hapa mahakamani kwa kile wanachoamini wao wanamakosa toka wamewashika hadi leo ambapo muda wa mahakama unakwisha na sisi tunataka kuondoka na kuona njia gani za kutuhakikishia usalama wa viongozi wetu,” amesema.

“Kwa maana hatuelewi sababu za kushikiliwa kwa viongozi wetu mpaka sasa maana tunaamini hawana makosa na kama wana makosa ni kwanini jeshi la polisi limeweza kuwashikilia viongozi wetu kwa takribani siku mbili ni kweli inawezekana wakati wakishikiriwa zilikuwa si siku za kazi lakini leo ni siku ya kazi ni kwani hawakuletwa mahakamani” amesema Sosopi.

Amesema inashangaza kuona jeshi la polisi likitupiga danadana kwa kutueleza kuwa watuhumiwa hao wataletwa lakini jambo la kushangaza hadi muda wakufunga mahakama umefika.

“Nataka kutoa wito kwa jeshi la polisi tumezungumza na jeshi hilo muda wote kwa lugha ya kizugu wanasema Polisi Huduma lakini kwa jeshi la polisi la Tanzania wanasema Polisi Force, jeshi hilo kwa sasa badala ya kuwa jeshi huduma ni jeshi kadhia.”amesema Sosopi.

Amesema jeshi la polisi lisipende kuendesha nchi kwa vitisho kwani alisema vijana wa chadema wanalieshimu jeshi hilo hivyo ni lazima litende haki.

Amesema jeshi la polisi lilikiendelea na vitisho hivyo Vijana wa Chadema watatafuta mbinu nyingine ya kuweza kupambana nao.
Kwa upande Fredy Kalonga, wakili wa Chadema amesema inaonesha wazi kuwa jeshi la polisi limevunja kanuni na katika na kuminya demokrasia jambo ambalo linasikitisha kwa chombo hicho Muhimu.
Amesema kitendo cha kuwanyima dhamana wateja wake ni kukiuka katika ya inchi kwani sheria inaelekeza wazi kuwa mtuhumiwa ianatakiwa kupelekwa mahakamani au kupatiwa dhamana.
“Wateja wangu nilikuwa nao tangu walipokamatwa na wameisha fanya kila jambo kwa maana ya kutoa maelezo lakini cha kushangaza tangu asubuhi saa moja na nusu tupo hapa lakini hakuna maelezo yoyote ni kwanini wateja wagu hawajaletwa mahakamani” amesema Wakili Kalonga.
“Kwa kawaida muda wa mahakama umeisha na sasa tunafuata taratibu nyingine za kipolisi ili kuweza kuwapatia dhamana “ amesema.
Baada ya dhamana kugonga mwamba wakili Kalonga alisema kitendo ambacho kinafanywa na serikali kupitia jeshi la polisi ni dalili za kuvunja katiba ka kuikandamiza demokrasia wazi wazi.
Chanzo Mwanahilisi Oline.