Zinazobamba

TGNP YAENDESHA MAFUNZO KWA MADIWANI KUHUSU BAJETI YENYE MLENGO WA KIJINSIA...YAWATAKA KWENDA KUSIMAMIA RASILIMALI VEMA


Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akifungua mkutano wa mafunzo ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia kwa madiwani zaidi 40 toka mikoa mbalimbali  hapa nchini. Mkutano huo ulifanyika katika kumbi za Mtandao huo uliopo Mabibo Jijini Daresalaam.


Baadhi ya Madiwani waliohudhuria mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo Bi Lilian Liundi.

Mmoja wa maafisa waandamizi wa Mtandao wa TGNP, akifafanua jambo katika mafunzo ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia kwa madiwani mbalimbali. Mkutano huo utakuwa wa siku 5.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tgnp Mtandao Bi. Lilian Liundi akiwasilisha mada kwa madiwani hao kuhusu hali ilivyo katika jamii. Lilian amesema hali sasa ni mbaya na kama bajeti haitapangwa kwa kufuata mlengo wa kijinsia hali itazidi kuwa mbaya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo ya siku tano.

Madiwani wakiwa makini kusikiliza mafunzo hayo