WAZIRI MPANGO AJITETEA MIZIGO KUPUNGUA BANDARINI,SOMA HAPO KUJUA
HATUA ya kupungua kwa mizigo inayotoka nje ya nchi
kwenye Bandari ya Salama haitokani na ongezeko la kodi,
Dk. Phillip Mpango, Waziri wa
Fedha na Mipango amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa madai kwamba, mizigo kutoka
nje ya nchi imepungua kutokana na ongezeko la kodi “kauli hii si ya kweli.”
Dk
Mpango ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa uorodheshwaji wa hisa kwenye
Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mpango
amefafanua kuwa, kuyumba kwa soko la China ndiyo sababu ya mizigo hiyo kupungua
kwa kuwa, Tanzania inashirikiana na nchi hiyo katika masuala ya kiuchumi.
“Muangalie
uchumi wa China unavyokwenda, soko lake limepungua ulimwenguni, kutokana na
sababu ya nchi kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na china kumeathiri. Kodi
haiathiri chochote kile, na kelele zote zinazoendelea zinafanywa na wale
wakwepa kulipa kodi.
“Waambie
waache porojo, waende kwenye takwimu, hata kwa nchi jirani ya Kenya mizigo
inayoingia imepungua kwenye Bandari ya Mombasa. Waende wakapate ripoti.”
Amesema
kuwa, serikali ipo makini na wafanyabishara ambao hawataki kulipa kodi. “Walipe
kodi tu ili serikali iweze kuwahudumia, haiwezekani bandari itoe huduma kwa
wafanyabiashara pasi na wao kulipa kodi, hapana.”
Kuhusu
hisa 20,250,000 zilizoorodheshwa leo katika soko la hisa la Dar es Salaam Dk.
Mpango amewataka wafanyabiashara wazawa kuitumia fursa hiyo kwa kununua hisa
hizo ili kukuza mitaji yao.
“DSE
iendeleze uboreshaji wa mfumo wa kiteknohama a soko ili kurahisisha ufikiwaji
wa soko la hisa kwa watanzania waliopo nchini na wanaoishi nchi za nje.
“Na
pia ningependa kuwahamasisha kuendelea kutumia ujio wa teknolojia mpya ya simu
ya mkononi ili kufanikisha lengo hili,” amesema Dk Mpango.
Nasama
Massinda, Kamishna wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) amesema,
ongezeko la kampuni zinazowekeza kwenye DSE litaisadia serikali kupata mapato
yake inavyostahili.
“Serikali
itapata mapato yake inavyostahili kwa sababu ili wawekezaji waweze kuwekeza
katika soko la hisa lazima mapato na soko lake liwekwe bayana na kwamba jambo
hilo litaiwezesha serikali kutoza kodi inavyostahili,” amesema.
Kuorodheshwa
kwa hisa 20,250,000 na DSE kunatokana na mauzo ya awali yaliyofanyika mnamo
tarehe 16 Mei hadi Juni 3 mwaka huu ambayo yamewezesha upatikanaji wa fedha Sh.
10,125,000,000 na kwamba, kuorodheshwa huku ni muhimu kwa kuwa kutawezesha
wawekezaji walionunua hisa katika soko la awali kupata fursa ya kuziuza na
kuruhusu wawekezaji wapya.