Zinazobamba

RC CHALAMILA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI ATANGAZA MKAKATI WA USAFI NA MIRADI MIPYA YA MAENDELEO DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila, ametangaza mkakati wa kuboresha usafi wa mazingira, kuimarisha usalama na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi katika Mkoa huo, ikiwemo uzinduzi wa kampeni maalumu ya usafi itakayofanyika Novemba 14, 2026 pamoja na kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya kwa wote

Akizungumza Novemba 6, 2026 Jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari RC Chalamila amesema Mkoa huo ni kitovu cha biashara na diplomasia hivyo inahitajika mipango madhubuti, hivyo kampeni ya usafi itakayozinduliwa katika viwanja vya Posta Kijitonyama Novemba 14 itakua na lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira ikihusisha pia ugawaji wa vifaa vya usafi na utoaji wa pikipiki kwa ajili ya kuratibu na kusimamia shughuli za usafi katika mitaa huku akieleza kuwa Dar es Salaam inazalisha takribani tani 4,657 za taka, hali inayohitaji uwekezaji mkubwa katika ukusanyaji na uchakataji wa takaAmeeleza kuwa Mkoa umepata mwekezaji kutoka nchini Ghana ambaye anatarajiwa kuwekeza katika uchakataji wa taka ili kuzalisha mbolea, hatua itakayosaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuongeza thamani ya taka.

Akizungumzia suala la wafanyabiashara wadogo Chalamila ametaja mipango ya kujenga masoko ya kimkakati katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Tandika na Mbagala, pamoja na soko litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara wadogo 14,000 katika eneo la Kigogoo sambusa akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuwapatia wafanyabiashara wadogo maeneo rasmi ya kufanyia biashara ili kuwawezesha kukuza shughuli zao huku wakizingatia sheria na taratibu za mipango miji.Katika sekta ya afya, Chalamila amesema Mkoa unaandaa kampeni ya kuhamasisha na kuongeza uelewa wa bima ya afya kwa wote ili wananchi waone umuhimu wa kujiunga ambapo wananchi wenye uhitaji watasaidiwa kupata bima kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali.

Aidha amezungumzia suala la amani na usalama wa mkoa huo ambapo amewataka wananchi nakuendelea kulinda amani, akieleza kuwa Dar es Salaam ni kitovu  cha uchumi, biashara na diplomasia nchini ambapo

amelaani vitendo vya ujambazi na uporaji vinavyohatarisha maisha ya wananchi, akitolea mfano wa kijana mfanya biashara kuuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa na silaha.

kampeni hiyo ya usafi itakayozinduliwa katika viwanja vya Posta Kijitonyama itakuwa na kaulimbiu isemayo “Dar es Salaam Safi Tushiriki Pamoja”, ikiwa na  lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira.



No comments