IKULU YA MAGUFULI YAKOSELEWA,NI KUHUSU UTEUZI WA WAKURUGENZI,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa ofisini kwake Ikulu |
UTEUZI wa Rais John Magufuli wa wakurugezi wa
halmashauri za majiji, manispaa, miji, wilaya na makatibu tawala wa wilaya
umekosolewa, anaandika Pendo Omary.
Ukosoaji huo unakuja baada ya
baadhi ya majina ya walioteuliwa katika nafasi hizo kuonekana zaidi ya mara
moja katika nafasi mbili tofauti, hatua inayotajwa kuashiria kutokuwepo kwa
umakini wakati wa uandaaji wa orodha ya majina hayo au uteuzi huo.
“Inashangaza!
ofisi ya rais ina watumishi wangapi hata kushindwa kuhakiki majina 200?
Kama
ofisi kubwa kiasi hicho inashindwa kuhakiki wateuzi hao, je nchi inawezaje
kuhakiki maelfu ya watumishi wa serikali yetu?” anahoji Eliud Ibrahim, mkazi wa
jijini Dar es Salaam.
Ibrahim
anasema, mara kadhaa Rais Magufuli na baadhi ya Mawaziri wamekuwa wakiwatia
“tumbo joto” ama kuwafukuza baadhi ya watumishi wa serikali kuhusu usahihi wa
taarifa wanazozitoa lakini wao wameonekana hawawezi kabisa.
“Tulishuhudia
kutenguliw kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ana Kilango Malecela baada
ya kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo
ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa
wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza.
“Lakini
pia tumeshuhudia zaidi ya mara moja Ikulu ikitoa taarifa kimakosa ikiwemo ile
ya uteuzi wa Emile Ntakamulenga ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya
Serengeti lakini alipofika Ikulu wakati wa kuapishwa akaambiwa uteuzi wake
ulikosewa. Nani anawajibika kwa uzembe huu?,” anasema Elizabeth Marunge., mkazi
wa Dar es Salaam.
Miongoni
mwa makosa yaliyofanywa na Ikulu jana ni uteuzi wa Dk. Leonard Massale ambaye
alitangazwa jana kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wakati tayari ni Mkuu wa
Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza
Hakuna maoni
Chapisha Maoni