DC KINONDONI ATEKELEZA AMRI YA RAIS MAGUFULI KWA VITENDO,TATIBU LUPIMA ATOA USHAURI KWA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
.
SERIKALI nchini imetakiwa kuhamishia nguvu
waliyotumia katika upatikanaji wa madawati kwenye shule mbali mbali nchini na kuelekeza katika ujenzi wa maabala na
madarasa ili kuweza kumaliza tatizo hilo kwenye shule mbali mbali hapa nchini.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Ombi hilo limetolewa na John Lupima ambaye ni Tabibu Bingwa wa tiba mbadala kutoka kwenye
kituo cha sayansi ya Tiba asili na tiba mbadala cha Lupimo Sanitarium Clinic wakati alipokuwa anakabidhi
madawati 50 yenye thamani ya milioni 7 katika Halmashauri ya Kinondoni.
Ambapo amesema kwa licha ya serikali kuwekeza nguvu
hadi kufanikiwa kukalibia kumaliza tatizo ukosefu wa madawati basi akaitaka
serikali kuhamisha nguvu hiyo kwenye kumaliza tatizo la ukosefu wa madarasa
pamoja na maabala ya kufundishia kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi jambo
analodai litaweza kuikuza elimu yetu.
Amesema kwa sasa kumekuwa na changoto kwenye baadhi
ya shule kukosekana kwa madarasa ya kufundishia pamoja na Maabala ya
kufundishia hadi kupelekea wanafunzi kufanya vibaya kwenye matokeo ya kidato
cha nne.
Amebanisha kuwa njia ya sahihi ya kuweza kuinua
elimu yetu na kuondoa changamoto ya wanafunzi kufanya vibaya kwenye matokea ni
serikali kuongeza bidii katika kutatua tatizo hilo.
Amesema hatua yake ya kusaidia madawati hayo
imetokana na jitihada alizozionyesha Rais John Magufuli aliyoiweka katika
kuhakikisha kuiboresha elimu hapa nchini
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally
Hapi amemshukuru Tabibu huyo kwa mchango wake aliutoa wa madawati hayo huku
akiwataka watu wengine wenye mapenzi ya kuisaidia elimu ya hapa nchini
wajitokeze katika kusaidia mchango wa madawati ili tatizo liweze kukamilika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni