Zinazobamba

LHRC YAONGEZWA NGUVU, YAPEWA DOLA ZAIDI YA 2 MIL....BALOZI WA NORWAY ASIFU JITIHADA ZAO



Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Anne-Marie Kaarstad  akibadilishana mafailli na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Bi. Kijjo Bisimba mara baada ya kutiliana saini msaada uliotolewa na Nchi ya Norway ili kukiwezesha kituo hicho kupigania haki za bidamu kwa ari. Nchi ya Norway imetoa Krone 17.5Mil.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Kijjo Bisimba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Anne-Marie Kaarstad akitia saini kuashiria makubaliano ya ufadhili huo.

Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia zoezi la utiliaji saini wa mkataba huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka 2016 hadi  2018.




Kituo cha sharia na haki za binadamu LHRC kimepata nguvu mpya ya kuendeleza mapambano ya haki za binadamu hapa nchini baada ya kufanikiwa kupata msaada wa Krone 17Mil sawa na dola Mil. 2.125 katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018 kwa ajiri ya uendeshaji wa miradi mbalimbali ya kituo hicho 

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kutiliana saini Makao Makuu ya Kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bi Kijjo Bisimba amesema Msaada huo umekuja wakati muafaka kwani bado kuna kazi kubwa ya kufanya ikiwamo kupigania uwepo katiba mpya na inayokubaliwa na wananchi wote.

Amesema katika kipindi hiki cha awamu ya Tano, kuna changamoto nyingi zinaanza kujitokeza lakini wamejipanga kuhakikisha wanatetea na kupigania haki za binadamu katika ardhi ya Tanzania na kwamba msaada huo utasaidia kuongeza ari kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Akizungumzia watu walionufaika na uwepo wa Kituo hicho toka kuanzishwa kwake, Bisimba amesema tayari ya wananchi 150,000 wameweza kufikiwa na kusaidiwa katika changamoto zao, hivyo ujio wa msaada huo utaongeza ufanisi wa kazi.

“Si mara ya kwanza Serikali ya Norway kusaidia Kituo chetu cha sharia na haki za binadamu, toka mwaka 2004 wamekuwa bega kwa bega na sisi, hawajatuacha gizani. Kwa kweli tunawashukuru sana kwa kutuamini na kuendelea kutupa nguvu ya kupambania haki za watu hapa Tanzania”Alisema Kijo Bisimba.

Kwa upande wake Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Anne-Marie Kaarstad amesifu jitihada zinazofanywa na Kituo cha sheria za kuhakikisha mapambano ya haki za binadamu yanaendelea bila woga, na kwamba Nchi yake imefurahisishwa na jinsi wanavyofanya kazi.

Amesema kufuatia hali hiyo, Nchi ya Norway imeamua kuendelea kufanya kazi na Kituo hicho kwa kufadhili shughuli zake, kwani wanaamini kupitia kituo hicho wananchi wengi wananufaika ikiwamo kupata haki zao walizodhulumiwa.

Hakuna maoni