Zinazobamba

BREAKING NEWS,YAMETIMIA SASA UKAWA WARUDISHA SHIRIKA LA UDA KWA WANANCHI,SOMA HAPO KUJUA



Pichani ni Meya wa Jiji,Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari



HATIMAYE Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameipora asilimia  51  ya hisa zilizopo katika shirika la Usafirishaji la Jiji la Dar es Salaam (UDA)  na kuzirejesha kwenye Mamlaka ya jiji hilo kutoka kwa mmiliki wa sasa hisa hizo, Kampuni ya Simon Group Limited ,

Baada ya kubainika kuwepo kwa udanganyifu  mkubwa katika umiliki huo wa hisa hizo na uuzwaji wake.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.


Hapo awali ,Halmashauri ya Jiji ilikuwa inamilikia asilimia 49 ya hisa huku Kampuni ya Simon Group Limited ilikuwa inamilikia asilimia 51,

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita amewaambia waandishi wa Habari leo Jijini hapa kuwa kikao cha madiwani kilichokaa mwishoni mwa wiki kimegundua kuwa  mnunuzi wa hisa hizo ambaye ni SGL haikufuata utaratibu katika mchakato katika kununua hisa hizo.

Ametaja makosa hayo ni kuwa uuzaji wa hisa hizo ulitakiwa uridhiwe na wanahisa katika kampuni lakini haikufanya hivyo jambo analodai ni kosa.

“Hakuna kumbukumbu zozote zainazoonyesha kuwa mwanahisa mwenza  wa Halmashauri ya jiji katika shirika la UDA  yaani msajili wa Hazina  kuridhia Halmashauri ya Jiji kuuza hisa kwa mtu mwengine nje ya wanahisa katika shirika la UDA”amesema Mwita.
Mwita ambaye pia nia Diwani wa Kata ya Vijipweni kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema hisa hizo pia ziliiuzwa bila ya kuzingatia sheria ya Manunuzi ya Umma (Puplic Procuremet Act) kutokana na Kampuni ya SGL haikuwa mwanahisa katika ununuzi wake wa hisa zisisogawiwa (Unaloloted shares) ulikuwa batili jambo analodai ndio maana hisa hizo alirudishiwa hiza zake lakini wao wanashangaa tena kampuni hiyo kupewa hisa hizo.

Sanjari na makosa hayo,pia Mwita ambaye ni meya anayeungwa mkono na Vyama vinavyounda Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi(UKAWA) ameendelea kutaja makosa yaliyofanywa katika uuzaji huo ni hatua ya kutofanyika kwa uthamini  wa mali za shirika la Uda kabla ya kuziliuza shirika hilo.
Amesema Baada ya Baraza la Madiwani kubaini upungufu huo wajumbe hao waliazimia kuwa fedha zilizolipwa kwa Halmashauri ya  jiji na Kampuni ya SGL kwa ajili ya kununua shirika  hilo zisirudishwe mpaka pale tathimini itakapofanyika na kujiridhisha kuwa kampuni  ya Simon haidaiwi kitu baada ya kubainika kuwa kampuni ya SGL ilitumia mali za uda kujunufaisha kwa malhai yake.
Hata hivyo,Madiwani hao wamependekeza kuwa kuundwa kwa kamati ndogo ili ifanye kazi ya uchunguzi wa kina kuhususiana na unaditilishaji wa uuzwaji hisa za Halmashauri ya jiji.
Mwita amewataja wajumbe wa kamati hiyo  ni Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe,Abdallah Mtolea ambaye ni mbunge wa Kinondoni pamoja na Jummane Mtinangi ambaye ni Mwanasheria wa Jiji.

Hakuna maoni