Zinazobamba

TSN SUPERMARKET/HYPERMARKET YAMWAGA “LOYALTY VOUCHERS’ KWA WATEJA WA MARA KWA MARA,SOMA HAPO KUJUA





Pichani ni Meneja Uhusiano na Masoko wa TSN Group, Jahu Kessy akitambulisha Vocha hizo zilizogaiwa Mwanza kwa Wateja. Afisa Mwajiri wa TSN Group Amos Paul akikabidhi Vocha hizo za punguzo la manunuzi ya bidhaa, kwa wateja wa kwanza kufurahia punguzo hilo TSN hypermarket Mwanza.




 

Pichani ni Meneja Uhusiano wa TSN Group, Jahu Kessy pia alieleza mpango wao wa kuendelea kuboresha biashara kwa kutangaza kwenye mitandao ya kijamii. Sasa unaweza kufollow TSN Group TZ kwenye mitandao ya kijamii kwa promotion mbalimbali zitakazoendelea kutambulishwa.


SASA unaweza ku’bargain’ kwenye supermarket, Meneja Uhusiano na Masoko wa TSN Group, Jahu Kessy ameelezea kuhusu mikakati ya kuboresha biashara za TSN kwa kutambulisha Loyalty Gift Vouchers kwa wateja.

Wateja sasa wanaweza kuomba na kupata punguzo la bei ya bidhaa walizonunua katika maduka yao yaliyopo, Kibo Complex-Tegeta, Bamaga Petrol station-Mwenge, Baraka Plaza-Mikocheni, Tancon House-Posta, Swiss Tower -Upanga Dar es Salaam pamoja na Rock City Mall-TSN Hyprmarket Mwanza iliyofunguliwa hivi karibuni.

Meneja Uhusiano huyo ambaye alizitambulisha Voucher hizo kwa mara ya kwanza Mwanza amewataka wateja kumiminika katika maduka yao kupata punguzo hilo la kwanza kufanyika katika supermartket. 

Alisema TSN inatoa punguzo la manunuzi kwa wateja wanaonunua bidhaa zisizopungua chini ya laki tatu ndani ya wiki moja. Alisema kupata punguzo la bei mteja atalazimika kujisajili na kuacha mawasiliano yake ya simu na kuhakiki mauzo yake kwa wiki. 

Katika promotion hiyo ambayo itadumu  miezi mitatu kuanzia sasa hadi mwezi wa saba, kwenye checkout point ya maduka ya TSN, utatakiwa kuomba kitabu na ujisajili kwa kuandika jina lako, kiasi cha manunizi uliyofanya na mawasiliano yako ukisubiri kufikia kiwango kinachostahiki ili uweze kukabidhiwa vocha hiyo.

Hakuna maoni