VIJANA WA CCM WAWAONYA WANASIASA WANAOPOTOSHA WANANCHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA MWAKA HUU.
Isack Sumbali (mwenye kofia) akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu upotoshaji kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba Mwaka huu.Na Mussa Augustine.
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam wamewaonya Wanasiasa na Wanaharakati wanaopotosha Wananchi wasishiriki Uchaguzi Mkuu kwa madai kuwa hakuna mabadiliko yaliyofanywa kwenye Sheria za Uchaguzi.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 24,2025,Makao Makuu ya UVCCM Jijini Dar es salaam,mmoja wa Vijana hao Isack Sumbali amesema kuwa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi yamefanyika kwa kiasi kikubwa ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kubadilishwa nakuwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC).
Aidha Sumbali amesema kuwa kwa sasa Uhuru wa Tume hiyo umeongezeka katika sehemu kuu mbili ambazo ni uhuru wa kitaasisi na uhuru wa kiutendaji,pamoja na kutungwa Sheria maalumu inayoongoza kupatikana kwa wajumbe wa tume tofauti na hapo awali wajumbe hao walikua wakiteuliwa na Rais.
Ameendelea kusema kwamba tume hiyo pia imekua na uhuru wa vyanzo vya mapato,hapo awali ilikua haiwezi kujiendesha kwa fedha za ndani,na kutegemea ufadhili kutoka UNDP, ambapo uchaguzi mkuu wa mwaka huu utagharamiwa na fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameongeza kuwa mabadiliko mengine ni pamoja mwaka huu kwa mara ya kwanza wafungwa waliopo Magerezani watapiga kura,hapo awali wafungwa Magerezani walikua hawafikiwi kujiandikisha kupiga kura,jambo ambalo linatokana na INEC kupewa uhuru mkubwa.
"Mabadiliko mengine ni kudhibitiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia kipind Cha uchaguzi,matumizi ya teknolojia wakati wa uboreshaji wa taarifa za mpiga kura,hivyo kupitia mabadiliko hayo uchaguzi utafanyika na pasitokee upotoshaji wa aina yoyote kuwa uchaguzi hautafanyika,kwani Serikali imefanya mabadiliko hayo ili kufanya Uchaguzi uwe wa haki."amesisitiza Sumbali
Mabula Marco Mabula(katikati waliokaa mbele)akizungumza na Waandishi wa habari( hawapo pichani).kushoto kwake ni Isack Sumbali na kulia ni Antipas Pamba.
Kwa upande wake Mabula Marco Mabula amewaomba Vijana wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge pamoja na kumpigia kura Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan.
" Kwa Vijana wa CCM watakaojitokeza kungombea nafasi hizo,chama chao kimewatengenezea utaratibu mzuri wa kushiriki nakuhakikisha wenye uwezo na sifa za kuongoza wanashinda"
Nakuongeza kuwa " miaka ya nyuma watu walikua wana nunua hizo nafasi,unakuta mtu anafedha anawahesabu kama njugu anawapa fedha,lakini chama chetu kimesema huo utaratibu hapana maana yake huwezi ukahonga zaidi ya watu elfu nane,hii ni hatua kubwa sana iliyofanywa na chama chetu".
Mabula amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi hakiko tayari kuachia nchi kwasababu wananchi wanaona maendeleo yaliyofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ametekeleza Ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 95.
Antipas Pamba(kushoto) akizungumza na Waandishi habari( hawapo pichani) na kulia kwake ni Mabula Marco MabulaNae Antipas Pamba amesema kwamba takwimu za Sensa ya Watu na Makazi zinaonesha asilimia 70 ya wakazi Nchini Tanzania ni Vijana hivyo kila jambo ambalo Serikali inalitekeleza wanufaika wakubwa wa jambo hilo ni Vijana.
Amesema kwamba yapo maeneo mahususi ambayo Serikali imeamua kugusa uchumi wa wananchi wa kawaida pamoja na Vijana,kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi.
"Serikali imeendelea kutoa ruzuku kwa kaya masikini,takribani shilingi bilioni 961.5 zimetolewa kwa watu wa kawaida wasiojiweza,pia Serikali imeghramia mpango wa Elimu bila ada kuanzia shule ya Msingi hadi kidato cha sita ambapo shilingi trioni 1.3 zimetumika katika mpango huo.
Aidha amesema kuwa Serikali imeendelea kutoa Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu na Vyuo vya kati,hadi sasa kiasi cha shilingi trioni 2.7 zimetumika katika mpango huo wa kusomesha watoto wenye hali ya maisha ya chini,pamoja na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 709 kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa Wakulima.
.jpg)

No comments
Post a Comment