SHEIKH PONDA AMPOPOA RAIS MAGUFULI,AIBUKA NA KUSEMA UTAWALA WAKE NI KULIPUALIPUA,SOMA HAPO KUJUA

SHEIKH Ponda
Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji
wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema una kasoro za
kiutawala, anaandika Happiness Lidwino.
Akizungumza na Mwanahalisi Online leo, Sheikh
Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.
“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini
lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:
“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu.
Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka. Watanzania watafurahi zaidi kama serikali
haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji
wake.”
Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za
wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti. Anasisitiza,
“jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na
inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.
“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka
madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam
mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Pond
No comments
Post a Comment