Zinazobamba

UTT AMIS INAENDELEA NA JITIHADA ZA KUWAFIKIA WAWEKEZAJI WA AINA ZOTE NCHINI: MIGANGALA


Na Mussa Augustine.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Serikali ya uwekezaji wa pamoja(UTT AMIS) Simon Migangala amesema kuwa taasisi hiyo inaendelea na jitihada za kuwezesha wawekezaji wa aina zote ili waweze kuzifikia fursa za uwekezaji.

Migangala amesema hayo leo Desemba 19,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Mkutano wa mwaka wa UTT AMIS,nakubainisha kuwa licha ya kuongezeka  kwa wawekezaji kwenye taasisi hiyo lakini bado Watanzania wengi hawajafikiwa na fursa hiyo.

"Leo tuna mkutano wa kwanza wa mfuko wa Umoja ambao watu wengi walijiunga mwaka 2005,mfuko huu umekua kwa kiwango kizuri sana,kwa sasa una Tsh. bilioni 400 lakini wakati unaanza ulifika bilioni 50,hivyo umeendelea kukua vizuri zaidi." 

Nakuongeza kuwa"Mfuko wa Umoja umekua na faida ya zaidi ya asilimia 12,mifuko mingine imekua kwa zaidi ya asilimia 13,na mingine imevuka asilimia 14,kuna mifuko miwili ambayo imevuka asilimia 15,kwa ujumla mwaka uliopita umekua mzuri sana." 

Amesema kuwa taasisi hiyo wakati inaanza ukubwa wa mifuko yote ilikua trioni 2.2 lakini mpaka wanafunga mwaka ulikua na trioni 3.2,hivyo kwa mwaka mmoja uliyopita wamekua na ukuaji wa zaidi ya trioni 1.

Aidha amesema kuwa kwa upande wa idadi ya wawekezaji pia mwaka huu umekua na ongezeko kubwa la wawekezaji kwa maana ya kwamba walipokua wanaanza walikua na wawekezaji takribani laki tatu,lakini mpaka sasa kuna wawekezaji zaidi ya laki tano.

"Tunashukuru wawekezaji wanaotumia huduma zetu za mifuko ya uwekezaji,lakini pia tunashukuru mamlaka na Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini kwasababu sisi(UTT AMIS )tunaopareti kwenye soko la mitaji." amesema 

Nakusisitiza kuwa "Kwa ujumla tunatambua kwamba watanzania wengi hatujawafikia lakini tunafanya jitihada za kuweza kuwafikia watu wengi zaidi,mwanzo hatukuweza kufika hata kwa wawekezaji elfu 10 kwa mwaka,lakini katika mwaka uliopita tumekua na wawekezaji wapya laki moja na elfu hamsini(150,000)."

Amebainisha kuwa Taasisi hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuwafikia Watanzania kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya kawaida ya kuongeza Ofisi Mikoani,ambapo katika mwaka uliopita imefungua ofisi maeneo mawili ambayo ni Morogoro pamoja na mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

"Pia tunatumia teknoloji,kwa sasa mifuko yetu imekua rahisi sana kuwekeza kwa mitandao yote ya simu ya hapa nchini,lakini pia tumefungua portal kwa maana mwekezaji akiwa na access kwenye mtandao anaweza kuendelea kuwekeza"amesema.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa bodi ya UTT AMIS Profesa Faustin Kamuzora amesema kwamba katika Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 suala la kuongeza kipato cha watanzania kutoka 1300/1400 za sasa za kila mtanzania mpaka dola kati ya 7500 hadi 8000 inahitaji ushiriki wa taasisi mbalimbali na taasisi za uwekezaji katika masoko ya fedha ni taasisi muhimu. 

"Katika suala la kuwaelimusha wananchi katika kuelewa elimu ya fedha taasisi yetu inajukumu hilo na tumejipanga tutakua na mazao mbalimbali,saivi tunayo mifuko saba lakini baada ya kuboresha mifumo yetu tunajiandaa kuwa na mazao mengine."amesema Profesa Kamuzora

Nakuongeza kuwa"katika kufika uchumi wa dola tirion 1, itakapofika mwaka 2050 kwakweli tunawategemea sana nyinyi Waandishi wa habari kuweza kutoa taarifa na maarifa kwa ajili ya kuboresha uwekezaji katika sekta ya fedha."  




No comments