TAMWA YALIA NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI,NI KUHUSU KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Pichani ni Mratibu wa kituo cha usuluhisho kutoka chama cha Wanahabari wanawake nchini,(TAMWA),Gladness Munuo (picha na maktaba) |
NA KAROLI VINSENT
OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)imetakiwa
kuharakisha haraka kesi zote zinazohusu makosa ya ukatili wa kijinsia ili kurudisha
imani ya wananchi katika Ofisi hiyo.
Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mratibu wa
kituo cha usuluhisho kutoka chama cha Wanahabari wanawake nchini,(TAMWA),Gladness Munuo wakati
wa mkutano wakutathimini mpango wa mradi wa kuangalia usawa wa kijinsia
kuwawezesha wanawake (GEWE),
Ambapo Munuo alisema kuwa kwa sasa ofisi ya AG
imekuwa ikichelewesha kesi zinazohusu ukatili wa kijinsi kwa hatua yake ya
kushindwa kuzipeleka mahakamani jambo analodai limechangia kuwakatisha tama
wananchi.
“Tumekutana hapa na watu wa idara mbali
mbali,wakiwemo Polisi,wanasheria na pamoja na wadau mbali mbali wa mambo ya kijinsia,tumejadili
kwa kina tumegundua bado kunashida katika ofisi ya Mwanasheria mkuu kwa
hatua yake ya kushindwa kwenda kwa kasi
kwenye kesi za ukatili wa kijinsia”alisema Bi Munuo,
Bi Munuo ametaka serikali kuishinikiza ofisi ya AG
kuziendesha kwa haraka kesi zinazohusu masula ya ukatili wa kijinsia ili
kuondoa malalamiko yanatolewa kutoka kwa waathirika wa vitendo hivyo ambao
wamekuwa wakikata tama kufika kutoa vitendo wanavyofanyiwa
.
Hata Hivyo,Bi Munuo ameleeza kuwa TAMWA na
kushirikiana na Taasis nyingine zinahusika na kupinga ukatili wa kijinsia
wataendelea kupambania harakati za wanawake kuhakikisha mwanamke anaheshimiwa.

No comments
Post a Comment