MABILIONI YA MCC YAIGAWA SERIKALI YA MAGUFULI,MAWAZIRI WAKE WAJICHANGANYA,SOMA HAPO KUJUA

SIKU mbili tangu
Marekani iifutie Tanzania misaada kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia,
viongozi wa serikali ya Tanzania wamekuwa na misimamo inayojikanganya, anaandika Happiness Lidwino.
Wakati Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na
Mipango, na Dk Servacius Likwelile, Katibu Mkuu wa wizara hiyo,
wakisema pesa za MCC hazikuwekwa kwenye bajeti sababu walijipanga baada ya
kuona dalili nyingi za kuzikosa, Balozi Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya
Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, amesononeka kwa Tanzania kukosa
msaada wa MCC.
Balozi Mahiga aliwaambia waandishi wa habari wiki hii Jijini Dar
es Salaam kuwa, hatua ya MCC inafuta imani na uelewano uliokuwepo kati ya
Tanzania na wahisani.
Alisema: “Suala la nishati ndio mradi wa maendeleo ya nchi hii,
hatuwezi kufanikiwa kwa chochote bila kuwa na nishati ya umeme, mfano ukienda
hospitalini vifaa vingi vinahitaji umeme, au shuleni.
“Wametufutia msaada pale ambapo maendeleo yetu yanaanzia, na ni
eneo ambalo linauma zaidi, wametuahidi pesa kisha wakaziondoa.”
Kauli ya Mahiga imepingana pia na ya Dk Lutengano Mwakahesya,
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA), ambaye ametamba
kuwa REA haitaathirika kwani hakuna msaada wala pesa yoyote wanayoitegemea
kutoka MCC.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwakahesya amesema REA
inategemea asilimia 90 kutoka serikalini na asilimia 10 kutoka kwa wahisani.
Amedai kwamba serikali haijawahi kupokea msaada kutoka MCC tangu mradi huo
uanze mwaka 2007.
Amesema wafadhili wanaochangia REA ni asilimia tatu (3%) na
kiasi kingine cha pesa hutoka Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania
(Tanesco).
“Wasambazaji na wazalishaji, hupata Tsh.100 kutoka
kwenye mafuta ya petrol, na Tsh.150 kwenye mafuta ya taa na
wahisani kutoka nje, lakini si MCC,” amesema Mwakahesya.
Ameongeza kuwa sheria ya nishati ya vijiji inasema
mzalishaji yeyote anatakiwa kuchangia REA asilimia tatu na wanapata
asilimia hizo kutoka kwa wazalishaji na wasambazaji.
Dk. Mwakahesya amesema tathimini ya usambazaji wa mradi wa
umeme vijijini hadi sasa inaonesha kuwa wamesambaza umeme huo kwa
vijiji 5200, sawa na asilimia 36.
Amedai nchi nzima ina vijiji 15,000 na umeme umefanikiwa kufika
vijiji hivyo, na bado wanaendelea na kazi hiyo.
Wakati mradi huu unaanza mwaka 2007 usambazaji wa umeme
vijijni ulikuwa ni kwa asilimia mbili. Wizara inadai kuwa sasa umefikia
asilimia 36.
Dk. Mwakahesya amesema kwamba mradi huo unakua na serikali
itafikia malengo ya kusambaza umeme katika vijiji vyote kama ilivyopanga.
Anadai hadi sasa imejenga transfoma 5000 nchi nzima bila kutegemea msaada wa
MCC.
Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa hadi Tanzania inafutiwa awamu
ya pili ya msaada huo mwanzoni mwa wiki hii, MCC ilikuwa imetoa Tsh. trilioni
1.18 katika awamu ya kwanza.
Fedha hizo, pamoja na mambo mengine, zilitumika kutengeneza
mtandao wa kilomita 3,000 za nyaya za umeme vijijini, na kilomita 450 za
barabara za lami ikiwamo ile ya Tunduma – Sumbawanga, yenye zaidi ya kilomita
240.
Awamu ya pili ya fedha hizo ilitarajiwa kuendeleza miradi ya
umeme vijijini na kujenga barabara za lami katika mikoa inayozalisha kwa wingi
vyakula na kuunganisha na maeneo mengine ya nchi, ili wakulima waweze kuuza
mazao yao.
Tarehe 29 Septemba mwaka jana wakati akiwa mgombea urais, John
Magufuli, akiwa katika Kata ya Mvumi, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, alisema
anawashangaa watu wanaokejeli safari za aliyekuwa Rais Jakaya Kikwete kwenda
nchi za nje, akisema zimeleta manufaa makubwa kwa taifa.
Miongoni mwa faida ambazo Magufuli alisema zimetokana na safari za
Rais Kikwete ni Tsh. bilioni 992 zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia
mfuko wa MCC kwa ajili ya miradi ya umeme kama sehemu ya matunda ya safari za
Rais Kikwete nchi za nje.
Alisema: “mabilioni yaliyotolewa na MCC, yatasaidia kusambaza
umeme katika mikoa na vijiji vingi nchini na tayari mipango imekamilika ya
kuwafikishia wananchi nishati hiyo.
No comments
Post a Comment