HATIMAYE SASA POLISI RUKSA KUUA,SOMA HAPO KUJUA
JESHI la Polisi limeamriwa kuua mtu yeyote ataedaiwa
kuwa jambazi, anaandika Moses
Mseti.
Ruhusa hiyo imetolewa leo na
Ahmed Msangi, kamanda mpya wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni
Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP).
Msangi
ambaye amehamia mkoani humo akitokea Mbeya, ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na maofisa usalama na polisi wa vyeo mbalimbali baada ya
kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo na SACP, Justus Kamugisha.
Msangi
ametoa kauli hio siku chache baada ya John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
kusema kwamba, Kamugisha alikuwa mzigo kwenye jiji hilo kutokana na kushindwa
kukabiliana na ujambazi.
Katika
kipindi cha miezi miwili ya Machi na Aprili mwaka huu, matukio saba ya uhalifu
wa kutumia silaha za moto umeripotiwa na katika matukio hayo watu sita
walipoteza maisha.
Msangi
amesema kuwa, anawashangaa polisi wanaoshindwa kutumia silaha zao kuwaua watu
wanaodaiwa kuwa majambazi na kusababisha vitendo vya uhalifu kuendelea
kushamiri jijini humo.
“Tumieni
na nyie bunduki zenu kuua watu ambao ni majambazi, haiwezekana uwe na silaha
halafu unaacha kuchukua hatua za haraka za watu ambao wanasababisha mauaji na
uporaji wa mara za raia,” amesema Msangi.
Msangi
amesema, Jiji la Mwanza miezi michache iliyopita limetikiswa na matukio ya
unyang’anyi wa kutumia silaha yanayoambatana na mauaji ya raia, kujeruhi na
uporaji wa mali zao.
Amesema
kuwa, polisi wanapaswa kufanya kazi zao kwa kujiamini na kuacha kufanya kazi
kwa mazoea.
Kamanda
Kamugisha akikabidhi ofisi hiyo aliwahimiza polisi kufanya kazi kwa weledi na
kwa kuzingatia maadili ya jeshi hilo bila kumuonea mtu yeyote yule.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni