BAJETI YA MAGUFULI YAZIDI ANDAMWA,HAKIELIMU WALIA NA WABUNGE,SOMA HAPO KUJUA
PIchani ni Mkurugenzi wa HakiElimu,John Kalage akizungumza na Waandishi wa habari leo mapema Jijini dar es Salaam |
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa imebakia siku nne ili kuanza Bunge la kujadili na kupitisha
Bajeti ya serikali ya mwaka 2016-2017,Teyari Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Hakielimu imewataka
wabunge kuondoa itikadi zao za vyama na kuungana pamoja ili kuishinika serikali
kupunguza fedha za matumizi ya kawaida
katika bajeti ya wizara ya elimu,
Ili fedha hizo za matumizi ya kawaida zielekezwa
kwenye mipango ya Maendeleo ya elimu.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam,Mkurugenzi Mtendaji-HakiElimu,John Kalage amesema wanawataka Wabunge
kuuungana na kuishinikika serikali kuetekeleza mpango wa miaka mitano
(2015-2020) unayoitaka bajeti ya kawaida na ya
maendeleo kuwa na uwiano wa asilimia 60 na 40.
Amesema Bajeti iliyopo hakizi hali harisi ya Elimu
na imechangia kurudisha maendeleo ya
elimu kutokana bajeti ya elimu kuwa ndogo,
Kalage ametolea mfano Bajeti ya Fedha ya mwaka
2015/2016 bajeti nzima ya elimu ilikuwa Bilioni 3,887.kati ya hivyo Bajeti ya
maendeleo ya sekta ya elimu ilikuwa
bilioni 604 tu sawa na (16%) ya
sekta nzima,huku bajeti ya matumizi ya kawaida ikiwa ni bilioni 3,282 sawa na (84%) ya Bajeti nzima jambo analodai ni
vigumu elimu yetu kukuwa kwa kuwa na bajeti hii.
Hata hivyo Kalage ameonesha masikitiko yake katika
Bajeti hiyo kwa kusema licha upangaji huo wa fedha inayodaiwa kuwa ni fedha ya
maendeleo katika sekta ya elimu huelekezwa katika kugharamia mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu,
“Kwa mfano Bajeti ya 2015/16 bajeti ya
maendeleo ilitengwa bilioni 604,lakini
nusu ya fedha hizo bilioni 306 ilitengwa
kwa ajili ya mikipo ya elimu ya juu,hivyo bajeti ya maendeleo ya elimu ilikuwa
Bilioni 298,sasa kwa hali hii elimu yetu haitaweza kukuwa “amesema Kalage.
Kalage ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali
kuondoa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu katika bajeti ya maendeleo
ya sekta ya elimu na badala yake amesema fedha
hizo zipangwe katika matumizi ya kawaida ,kwa madai kuwa itasaidia kutoa
picha halisi ya matumizi ya maendeleo katika sekta ya elimu.
Katika hatua nyengine,HakiElimu pia wamewataka
Wabunge kuitazama kwa umakini dhana ya elimu bure iliotengwa na Rais John
Magufuli kwa kuangalia bajeti husika inayokwenda kutekeleza elimu bure kwa
madai kuwa Bajeti iliyopo ni ndogo kabisa na hakikizi maitaji harisi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni