Zinazobamba

BILIONEA LUGUMI HAKAMATIKI,ACHEZEA SHARUBU ZA SERIKALI YA MAGUFULI,NI YULE WA BILIONI 37 ZA JESHI LA POLISI,SOMA HAPO KUJUA



 

SAID Lugumi ambaye ni mmilikiwa Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo imengia mkataba tata wa zaidi bilioni 37 na Jeshi la Polisi imebainika mtu huyo  hakamitiki na Serikali ya Rais John Magufuli baada ya kuwa na mtandao mkubwa ndani ya serikali yake.(Mtandao huu umedokezwa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Lugumi ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kupindukia katika kipindi kifupi, aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Serikali ambazo Fullhabari.blogs imezipata zinasema Lugumi anamtandao ndani ya serikali ya Rais Magufuli ndiyo sababu  iliyopia jeuri jeshi la Polisi kuigomee Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambayo  ili utaka mkataba huo.

“Tatizo lenu wanahabari mnafikilia huyu Lugumi ni mtu mrahisi kama mnavyomfikilia nyie,nakwambia huyu mtu si wa kawaida,na huo mkataba ameingia kutokana na kupewa Baraka na wakubwa,wengine wapo kwenye nafasi za juu za serikali iliyopo madarakani,ndio maana yeye mwenyewe anajiamini na hata hilo jeshi la polisi linamgwaya mtu huyo”kimesema Chanzo chetu kilichopo ndani ya serikali.

Katika mkataba huo, Kampuni ya Lugumi ililipwa kiasi Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba, lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee jijini Dar es Salaam ambavyo hata hivyo haijaainishwa maeneo vilipo,kwa mujibu wa taarifa mbali mbali zinasema kati ya mashine hizo 14 ni mbili tu zinazofanya kazi.

 Mkataba huo wa Polisi na Lugumi umezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kunyang’nywa hoja hiyo na badala yake kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.

Kutokana na hali hiyo, hadi kufikia Jumatatu saa 10 jioni, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi, ambapo kamati hiyo ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo hadi kufikia leo.
 TAARIFA ZA KUTOROKA ZASHIKA KASI
Licha ya Kamti ya Bunge kuutaka mkataba huo,kuna taarifa ambazo zipo zinasema Mfanyabiashara huyo Lugumi ameondoka nchini na haijafahamika wapi ameelekea.
Taarifa zilizowanukuu watu wake wa karibu zinasema Lugumi ametimkia kwenye moja huku balani ulaya kwa ajili ya mapumziko na kuchana na kile kinachodaiwa ni "kuchoshwa na vyombo vya habari" .

Hakuna maoni