ZITTO KABWE NA MBUNGE BASHE WAJIUZULU RASMI,NI BAADA YA WABUNGE WA CCM KUPOKEA RUSHWA NJE NJE,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameishtumu
Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe
wammepokea rushwa.
Kutokana na shtuma hizo ameamua kumuandikia spika barua ya kujiuzulu na kumtaka achunguze na kuchukua hatua.
Hii ni nakala ya barua yake aliyomwandikia spika wa bunge
Mbunge wa Nzega Mjini na Kiongozi wa chama cha CCM, ameishtumu Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe wammepokea rushwa.
Kutokana
na shtuma hizo ameamua kuungana na Zitto Kabwe kumuandikia spika
barua ya kujiuzulu na kumtaka achunguze na kuchukua hatua.
KAMATI za Kudumu za Bunge zinatarajiwa kufanyiwa
mabadiliko makubwa ya viongozi na wajumbe wake wakati wowote kuanzia sasa,
baada ya ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa wabunge kuwatuhumu baadhi yao
kujihusisha na vitendo vya rushwa kutua mezani kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Taarifa za uhakika zilizolifikia MTANZANIA kutoka
ndani ya Ofisi ya Bunge, zinaeleza kuwa Spika Ndugai atawang’oa katika nyadhifa
za uenyekiti na makamu wenyeviti wa watano wa Kamati za Bunge kutokana na
tuhuma hizo za rushwa.
Hatua hiyo ni pamoja na kuhawamisha baadhi ya
wabunge kutoka kamati moja hadi nyingine, kutokana na majina yao kutajwa na
wengine kuhusishwa moja kwa moja na tuhuma za rushwa.
Imeelezwa kwamba, Spika Ndugai amelazimika kuchukua
uamuzi huo baada ya kufikishiwa mezani ripoti ya uchunguzi uliofanywa na
taasisi za kiuchunguzi za Serikali, kuhusu mwenendo usioridhisha wa baadhi ya
wabunge hususan waliopewa dhamana ya kuongoza Kamati za Bunge.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wenyeviti wa Kamati za
Kudumu za Bunge wanaotajwa kuvuliwa nyadhifa zao wakati wowote kutokana na
tuhuma hizo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Martha Mlata ambaye
ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM).
Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na
Mitaji (PIC), Richard Ndassa, ambaye pia ni Mbunge wa Sumve (CCM) na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Dk. Mary Mwanjelwa
ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM).
Makamu wenyeviti wanaotajwa kuwamo katika orodha ya
kuondolewa katika nyadhfa zao ni Dk. Raphael Chegeni (Kamati ya Huduma za
Maendeleo ya Jamii) ambaye pia ni Mbunge wa Busega (CCM), Mbunge wa Mwibara,
Kangi Lugola (CCM), Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Vyanzo vya habari vya gazeti hili kutoka ndani ya
Ofisi ya Bunge vimeeleza kuwa Spika Ndugai baada ya kufikishiwa ripoti yenye
tuhuma dhidi ya baadhi ya wabunge, aliwaita ofisini kwake, wenyeviti wa kamati
watatu ambao ni Mlata, Ndassa na Dk. Mwanjelwa pamoja na makamu wenyeviti
wawili ambao ni Lugola na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM),
ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).
Wabunge kadhaa wamelieleza gazeti hili kuwa sakata
hilo limelitikisa Bunge kiasi cha kumlazimu Spika kuwaonya wenyeviti na makamu
wenyeviti aliokutana nao ofisini kwake kuhusu nyendo zao baada ya majina yao
kutajwa kwenye ripoti hiyo wakidaiwa kujihusisha na rushwa, huku Aeshi ambaye
jina lake halimo kwenye orodha ya watuhumiwa akitakiwa kuwa makini yeye
mwenyewe pamoja na wajumbe wake, kwa sababu kamati anayoingoza imekuwa
ikikumbwa na tuhuma za namna hiyo kila mara.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya Ofisi ya Bunge
zimeeleza kuwa katika ripoti aliyokabidhiwa Spika Ndugai, kuhusu mwenendo
usioridhisha wa baadhi ya wabunge, zimetajwa baadhi ya taasisi za umma ambazo
zimekuwa zikiombwa au kushinikizwa kutoa rushwa.
Taasisi zilizotajwa ni Shirika la Ugavi wa Umeme
Tanzania (TANESCO), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
Ofisa mmoja wa juu wa Bunge (jina tunalifadhi)
amelieleza gazeti hili kwamba uchunguzi umebaini kuwa, Mlata akiwa na mmoja wa
wajumbe wa kamati yake anatuhumiwa kupokea kiasi cha Sh milioni nane kutoka
Ewura.
Huku akilionyesha gazeti hili ripoti hiyo, alisema
uchunguzi umeonyesha kuwa Kamati ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii ilimtuma
katibu wake ambaye ni mtumishi wa Bunge kwenda kuchukua mzigo wa kamati hiyo
katika ofisi za NHIF, lakini alipofika alikabidhiwa mfuko uliojaa fedha ambazo
alikataa kuzipokea.
Alisema, ofisa huyo alirudi na kuitaarifa kamati
hiyo ameshindwa kuchukua mzigo huo kwa sababu ni fedha jambo ambalo haruhusiwi
kwa mujibu wa tararibu za kazi zake.
Ofisa huyo alisema, baada ya taarifa hiyo katibu
huyo alishambuliwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kwa kuwaangusha, huku
wakimuapiza asiseme jambo hilo na kwamba watazifuata wenyewe.
“Hawa jamaa sasa wanaomba rushwa wazi wazi na kwa
nguvu, wanatumia kamati hizo kuwabana na kuwatisha watendaji ili wawape
chochote, ripoti hii inamtaja Mlata kuwa alipokea shilingi milioni nane akiwa
na mbunge mwenzake na kamati ya Chegeni nayo ilimtuma katibu wake ambaye ni
ofisa kwenda kuchukua mzigo, lakini alipofika huko akakuta ni furushi la hela.
“Yule kijana alikataa kuzichukua kwa sababu maadili
yake ya kazi yanamzuia, akarudi akawaambia ameshindwa kuchukua mzigo wenyewe
kwa sababu ni furushi la hela, wakamfokea huku wakimwapiza asitoe siri hiyo na
kwamba watazifuata wenyewe, yeye alipotoka hapo akaenda kuripoti kwa mabosi
wake,” alisema ofisa huyo wa Bunge.
Spika Ndugai alipotafutwa kuthibitisha taarifa hizo
hakuweza kupatikana. Hata hivyo, Katibu wake, Said Yakub aliliambia gazeti hili
kwamba bosi wake anao utaratibu wa kuacha milango wazi kwa wabunge kukutana
naye mara kwa mara kwa ajili ya kujadiliana mambo ya kibunge na yale yanayohusu
utawala.
Alisema ni kweli kulikuwa na kikao hicho baina ya
Spika na wabunge hao lakini hawezi kuzungumza kilichojadiliwa isipokuwa Spika
mwenyewe ambaye ana mamlaka ya mwisho kuhusu uendeshaji wa shughuli za Bunge.
“Swali lako bwana mimi siwezi kulizungumzia sana,
unajua Spika ana utaratibu wa kuacha milango kwa wabunge wake ambao hukutana
naye mara kwa mara kwa ajili ya kujadiliana mambo ya kibunge yakiwemo ya
kiutawala.
“Sasa ni kweli wabunge hao unaowataja ambao ni
viongozi wa kamati walikutana na kufanya kikao na Spika lakini mimi siwezi
kukuambia kilichoongelewa humo ndani isipokuwa yeye mwenyewe kwa sababu ndiye
mwenye mamlaka ya mwisho ya kuhusu uongozaji wa Bunge,” alisema Yakub.
Alipoulizwa Dk. Mwanjelwa kuhusu jina lake kutajwa
kwenye tuhuma hizo alisema ni tuhuma ambazo hazina ukweli na kwamba nafsi yake
ni safi kwa sababu hajapewa fedha na mtu wala taasisi yoyote.
Dk. Mwanjelwa alikiri yeye pamoja na baadhi ya
wenyeviti wa kamati kuitwa ofisini kwa Spika ambao aliwaeleza kuwepo kwa maneno
mitaani kuhusu baadhi ya wabunge wanavyotumia majina ya wevyeviti kuomba rushwa
na kuwataka kuwasimamia vizuri pamoja na kuwafikishia ujumbe wa kubadilika.
“Ni kweli Spika alituita, mimi na wevyeviti wenzangu
wa kamati sita ambazo huwa zinakumbwa na majaribu sana. Alitutaka kuwa makini
kwa sababu ya unyeti wa kamati zetu lakini hakutuhumu kamati yoyote wala
mwenyekiti wa kamati yoyote kupokea wala kuomba rushwa,” alisema Dk. Mwanjelwa.
Kwa upande Mbunge wa Mwibara, Kangi alipoulizwa
kuhusu hilo, kwanza alieleza kushtushwa kwake na kuona habari inayohusu Bunge
kutikiswa na rushwa kisha akakanusha Spika kuzungumzia jambo lolote kuhusu
rushwa kwa wabunge.
“Mimi kwanza leo (jana) asubuhi nimeshtushwa sana na
taarifa niliyoona kwenye gazeti lenu ikihusu Bunge la rushwa, kikao kweli Spika
alituita lakini ni utaratibu wake wa kawaida kukutana na wabunge wake ila
kwenye kikao hicho Spika hakuzungumza lolote kuhusu rushwa hata kama inatajwa
mtaani hakuna ni uongo, kungekuwa na jambo kama hilo mimi ningekuambia,”
alisema Lugola.
Naye Mwenyekiti wa Kamati wa Nishati na Madini,
Martha Mlata, alipoulizwa alisema ni kweli Spika aliwaita baadhi ya wevyeviti
wa Kamati za Bunge ambazo alizungumza nao mambo mengi ikiwamo suala la kuwataka
na hata kuwaonya wajumbe wa kamati zao kuwa makini na kazi zao na kujiepusha na
vitendo vya rushwa.
Alipoulizwa kuhusu tuhuma anazoelekezwa za kupokea
Sh milioni nane akiwa na mbunge mwenzake alikanusha kwa kueleza kuwa tuhuma
hizo ni za uongo zenye lengo la kumchafua.
Mbali na hao, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma
na Maendeleo ya Jamii, Dk. Raphael Chegeni naye alikanusha yeye mwenyewe
na wajumbe wa kamati yake kujihusisha na rushwa na kueleza kuwa jambo hilo lina
nia ya kupunguza makali yao ya kuwasulubu watendaji wa Serikali wanaoshindwa
kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.
“Hatujaitwa kwa Spika, hatujachukua rushwa kwa mtu
yoyote. Hili lina lengo la kutupungumzia makali kwa sababu kamati yangu ina
watu makini na imekuwa ikiwindwa sana, unajua sisi tunawasulubu kweli kweli
watendaji wa Serikali ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao sawasawa, sasa kama
wameamua kutuchafua hilo litakuwa jambo jingine,” alisema Chegeni.
Alipoulizwa kuhusu kamati yake kutajwa kumtuma
Katibu wake kufuata mzigo NHIF, Chegeni alisema jambo hilo halina ukweli
wowote.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC), Richard Ndassa ametakiwa kufika leo
makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), baada ya
kuitwa kwa ajili ya mahojiano.




No comments
Post a Comment